Nafasi Ya Matangazo

July 29, 2011

Picha zikionesha magari  mawili Fuso lenye namba za usajili T 884 BFL (chini) na basi la  abiria mali ya kampuni ya Lim lenye namba za usajili T 489 BJR (kushoto) ambalo lilikuwa limebeba wafanyakazi wa kuchuma kahawa Tchibo Estate  na kugongana uso kwa uso Jana Julai 28, 2011 majira ya saa moja usiku na kuua watu 11 na kujeruhi 24 eneo la  Barabara ya Kibosho njia kuu ya Arusha - Moshi.
 Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo anasilumulia chanzo cha  ajali hii gari la FRESH COACH.
Ilikuwaje. "Basi la FRESH lilishusha abiria pale Kibosho road, ghafla akaingia barabarani. Driver wa LIM  alikuwa anatokea Moshi Mjini. Kwa wale wanaojua Moshi, ukitoka Moshi Technical Kuna muinamo ambao ni mkali. So gari ya Lim ikawa imekolea mwendo ndipo Fresh akaingia barabarani hivyo kumlaziimu huyu wa LIM kukwepa Fresh.
 Gari iliyokuwa ikitokea Uelekeo wa Arusha aina ya Prado ilibidi itoke nje ya barabara kabisa ili kukwepa LIM lakini pia aligongwa ingawa hakuumia sana. FRESH naye alitoka nje ya barabara! Wakakwaruzana ubavuni! 
Bahati mbaya sana fuso iliyokuwa inatokea uelekeo huo huo wa Arusha likiwa na shehena ya nyanya lilikutana uso kwa uso na basi hili dogo lililokuwa na wafanyakazi walioukuwa wametoka kuchuma kahawa pale Tchibo Estate. Ni bahati mbaya sana kuwa karibu watu wote wanatoka pale Machame. 
Ni msiba mkubwa sana. Tunaamini Mungu atawaongoza wote waliopoteza ndugu zao. Lakini anasema: Kwa wale wafanyabiashara wa break down. Nawatahadharisha sana wasitumie mianya ya ajali ili kujipatia fedha! Kuna break down moja jana iliwaudhi wananchi pale! Huyu jamaa inasadikika kuwa hulipwa kwa masaa! hivyo alikuwa anajichelewesha maksudi ili masaa yaende. 
Hakujali kuwa kuna watu wamekwama kwenye foleni au hata wagonjwa walio kwenye magari wakisubiri magari yaondolewe barabarani. Ilibidi mwananchi mmoja amfokee huyu mwenye break down. Huyu jamaa mwenye asili ya kihindi alikuwa anavuta sigara na kujidai kuwa anashughulika saana wakati hakuwa akifanya chochote.
Baada ya karipio kali toka kwa huyu raia ingawa hata polisi walikuwepo alivuta gari haraka na kulitoa barabarani na kisha kuondoka eneo la ajali na kuacha yale magari pale!
Hii nasema kwa ndugu zangu wa Musa Engineering hawakutenda haki!
Posted by MROKI On Friday, July 29, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo