Huu ndiyo muonekano wa kiwanda cha Kampuni ya bia ya Serengeti mjini Moshi katika mkoa wa Kilimanjaro kilichozindua rasmi usambazaji wa bia zake mara baada ya kuanza uzalishaji jioni ya leo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa usamabazaji wa bia za Serengeti Lager, zinazozalishwa na kiwanda hicho kipya katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro na vitongoji vyake ikiwemo na mikoa ya jirani ,uliofanyika jioni ya leo ambapo uzinduzi huo uliambatana na msafara mkubwa wa magari uliozunguka katikati ya mji wa moshi huku msafara huo ukiongozwa Mkurugenzi huyo, Richard Wells,sambamba na wafanyakazi wa kampuni hiyo,shamra shamra hizo zilinogeshwa zaidi wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipoamua kugawa bure kinywaji hicho cha Serengeti katika maeneo mbalimbali.
Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Lager,Allan Chonjo pamoja na wafanyakazi wenzake wakishangilia mara baada ya uzinduzi rasmi kufanyika jioni ya leo kiwandani hapo,mjini Moshi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Serengeti wakiwa bize jioni ya leo mara baada ya uzinduzi rasmi.
Pichani kati alienyoosha mkono juu ni Mkurugenzi wa kampuni ya Serengeti Breweries (SBL),Richard Wells akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa idara ya usambazaji kabla ya kuondoka kiwandani hapo jioni ya leo.
Pichani ni msafara wa magari ukikatiza katikati ya mji wa Moshi jioni ya leo kuashiria kuwa tayari bia aina ya Serengeti imeanza rasmi kuzalishwa ndani ya mji huo kwa wateja wao.Magari hayo yalikuwa yamepambwa kwa maandishi makubwa 'Kiwanda chetu,Bia Yetu !
0 comments:
Post a Comment