Nafasi Ya Matangazo

June 12, 2011

 Ukipita barabara kuu ya Morogoro Dodoma na ukaupita kidogo mji wa Gairo, iwapo unatokea Morogoro na kabla hujafika Gairo mjini kama unatokea Dodoma, utaliona jengo zuri la kiasili lililojengwa kwa ufundi mkubwa na kuezekwa kwa nyasi mkono wako wa kushoto au kulia. Basi hapo utakuwa umefika DOUBLE HOTEL na hakika ukiingia hapo ukiwa na usafiri binafsi au basi la abiria utafaidi vinono kwa kula au kuangalia mandhari.
 Magari husimama hapo, na abiria kujipatia chochote, kama vile wale waendao Arusha wanapoingia Pale Korogwe na Mombo, au Iringa na Mbeya wanapo ingia Confort au Aljazira. Na sasa Dodoma na Singida hata Tabora na Shinyanga hadi Mwanza wanaingia Gairo.
 Shabiby na Mohamed Trans niliyakuta hapa...
 Jikoni upande wa nyama choma ni super...
 Jengo kuu la Faal;agha nalo linavutia...
 hii inaashiria chai pia waweza ipata hapa...
 Wasafiri walipapenda...
Nami Father Kidevu japo sikula maana huwa sina desturi ya kula safari fupifupi nilienda kufurahisha macho.
Posted by MROKI On Sunday, June 12, 2011 1 comment

1 comment:

  1. Kuna VYUMBA hapo Mkubwa mwenzangu?

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo