Nafasi Ya Matangazo

May 24, 2011

TUMBAKU YA TANZANIA YAPATA SOKO CHINA
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami akifafanua jambo katika Mkutano huo.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami akiwasikiliza wageni wake (Kushoto)  wakieleza mikakati yao katika biashara ya kununua Tumbaku nchini. Kulia ni baadhi ya maofisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami ( Kulia) akiagana na kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China Bw Zhu Jineng, mara baada ya mazungumzo yao ofisi kwake.




Tumbaku inayozalishwa nchini Tanzania imepata soko nchini China na kuondoa wasiwasi wa kukosa soko uliotanda miongoni mwa wakulima wa zao hilo katika mikoa mbali mbali.


Habari hiyo njema kwa wakulima wa Tumbaku imebainishwa Jijijini Dar es salaam leo na ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka nchini China wenye nia ya kununua Tumbaku hiyo, walipomtembelea Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyrill Chami ofisini kwake.


“Sisi ni wafanyabiashara, tumepokea ombi la serikali ya Tanzania kupitia kwako Mh Waziri wa Viwanda na Biashara ulipowasiliana na Ubalozi wetu kuhusu kutafuta soko la Tumbaku kutokana na mavuno mazuri waliyopata wakulima wenu. Kwa kuanzia, tunao uwezo wa kununua tani elfu 60 za tumbaku ya Tanzania, tunaomba serikali zetu ziwasiliane na kutuwezesha kufanikisha mpango huu” amesema Bw Zhu Jineng, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao kutoka China.


Akijibu maombi hayo, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami amesema, serikali ya Tanzania itaunga mkono mpango huo ili kuinua hali za wakulima wa zao la tumbaku nchini. Ameongeza kuwa, pamoja na kupata soko la nje, serikali pia itaendelea kuvilinda Viwanda vya ndani ili vipate malighafi ya kutosha kuviwezesha kuendelea na uzalishaji na kuchangia pato la Taifa.
Posted by MROKI On Tuesday, May 24, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo