Nafasi Ya Matangazo

May 17, 2011

 Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka  jiwe la msingi katika , Shule ya Msingi Simai iliyopo Kijiji cha Wingwi Mapofu, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akiwa kwenye Ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo katika Miikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba leo Mei 17.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Simai, iliyopo Kijiji cha Wingwi Mapofu, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakiwa katika hafla ya kumpokea Makamu wa Rais.
 Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wanafunzi wa Shule ya Msingi Simai iliyopo Kijiji cha Wingwi Mapofu, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
 Makamu wa Rais  Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akikagua jengo la ofisi ya CCM ya Tawi la Majenzi iliyopo Kijiji cha Kusale, Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba leo Mei 17
Baadhi ya wanachama wa CCM na Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia alipowatembelea akiwa katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika mikoa ya Kaskizini na Kusini Pemba, leo Mei
Posted by MROKI On Tuesday, May 17, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo