Nafasi Ya Matangazo

April 04, 2011

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Hussein Bashe (kushoto) akizungumza na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Nembo ya Rangi Nyekundu ya kampuni hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kempinsk Dar es Salaam jana. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Vodacom, Dietlof Mare
 Mwanamuziki Karola Kinasha, akiimba jukwaani na bendi yake wakati akitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
 warembo waliokuwa wakitoa huduma ya kukaribisha na kuelekeza wageni kwenye hafla hiyo, wakipozi kwa picha.
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya simu za mkononi Vodacom, Dietlof Mare, akizungumza kuelezea maudhui ya nembo ya rangi nyekundu ya Vodacom.
 Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi wa Vodacom.
 Wasanii wa kikundi cha Ngoma cha Aficanashe, wakitoa burudani jukwaani, wakati wa uzinduzi huo.
 Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari walioahudhuria hafla hiyo 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa katka hafla hiyo wakifuatilia kwa makini kilichokuwa kikiendelea jukwaani.

Vodacom yaja upya na nembo ya rangi nyekundu



Dar es Salaam, April 3, 2001: Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania leo imezindua Nembo yake mpya kuashiria mabadiliko makubwa ndani ya kampuni hiyo na utendaji wa shughuli zake nchini.


Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom ambayo ni kampuni kubwa ya simu za mkononi nchini Dietlof Mare alisema kuwa mabadiliko hayo ya kwanza na ya aina yake kufanywa na Vodacom yataibadili nembo yake kutoka rangi ya bluu ya sasa na kuwa na Rangi Nyekundu na kwamba zoezi hilo linakusudia kuongeza ubora wa bidhaa na huduma zake.


“Naamini mabadiliko lazima yaanzie kwetu. Tunajipanga upya bila kupoteza thamani bali kuongeza ubora wa bidhaa na huduma zetu," alisema Dietlof Mare.

Mare alifafanua kuwa mabadiliko hayo yanalenga sio tu kuwapa wateja wa Vodacom huduma bora zaidi, lakini pia ya haraka kuweka hai na kutimiza ahadi ya kampuni hiyo kwa wateja wake kutoa huduma kulingana na thamani halisi ya fedha za wateja.


"Haya si mabadiliko ya nembo na rangi zetu pekee, bali kampuni nzima na jinsi inavyofanya biashara na kuhudumia wateja wake. Ni mabadiliko makubwa kuliko ya rangi, ni mabadiliko ya mtazamo na mwelekeo kwa Vodacom katika zama mpya ambapo mawasiliano si anasa tena bali ni hitaji la msingi,”alisema Mare na kuongeza:


“Tunataka kuunganisha nchi nzima kwa mawasiliano ya Vodacom, si mijini pekee bali maeneo yote hata vijijini na haya ndiyo mabadiliko tunayolenga na tunayowaletea."


Alisema mtandao wa kampuni yake, huduma na thamani ni maeneo matatu muhimu yanayogusa wateja wa Vodacom ambayo yamekuwa yakiboreshwa kwa nyakati tofauti pia ni sehemu ya hatua hizo za mabadiliko ndani ya Vodacom.


Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa sasa ndiyo yenye mtandao mpana zaidi nchini ambapo Mare amesema kuwa wanakusudia kuongoza katika teknoloji na kwamba mabadiliko ya teknolojia yataendelea kuwa sehemu muhimu ya Vodacom kuboresha mtandao wake pamoja na kuendelea kuongoza katika utoaji huduma za fedha kwa simu za mkononi nchini.

Alieleza kuwa Vodacom kama kampuni inayoongoza, inategemea kutimiza matarajio ya wateja wake kwa kutimiza ahadi zake akieleza kuwa mabadiliko yanayoshuhudiwa sasa ni mwanzo wa safari ya mabadiliko makubwa akiahidi kwamba Vodacom itafanya kazi zake kwa kuzingatia sheria, taratibu, uaminifu na kasi ya ajabu.


Mabadiliko hayo yamekuja kufuatia kampuni mama ya Vodafone Group (UK) ya Uingereza kununua asilimia 65 ya Hisa za kampuni ya Vodacom Group (SA) ya Afrikakusini na kuamua Vodacom kutumia nembo ya Vodafone na kauli mbiu ya "Nguvu Kwako"


Mabadiriko hayo ya rangi yataiwezesha Vodacom kuonekana uhalisia wake wakuwa kampuni tanzu ya Vodafone ambayo ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza katika nyanja za mawasiliano duniani kote.
Posted by MROKI On Monday, April 04, 2011 1 comment

1 comment:

  1. Bwana Mroki huyo anaitwa KAROLA Kinasha na sio FLORA Kinasha bwana

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo