Nafasi Ya Matangazo

February 01, 2011

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Precision Air, Alfonse Kioko (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo juu ya uzinduzi wa safari za Bukoba. Kulia ni Mkurugenzi wa Mipango wakpuni hiyo, Patrick Ndekama.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Dar es Salaam Jumanne, Februari mossi 2011 Mkurugenzi Mtendaji wa Precision Air Bw. Alfonse Kioko alisema;

“Tuanyo furaha kuwafahamisha wateja wetu kua tunaaza tena safari za kwenda Bukoba kuanzia tarehe 12 Februari baada ya kusitisha safari hizo kwa zaidi ya mwaka.”

Uzidnuzi wa safari hizo unafuatia kumalizika kwa ukarabati wa kiwanza cha ndege cha Bukoba uliofanywa na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.

“Huduma ya safari itakuwepo kila siku kutoka Dar es Salaam kupitia Mwanza na kutoka Bukoba kwenda maeneo tofauti katika mtandao wetu,” alisema Kioko.

“Tunaanza na bei ya Tshs. 454,000 kwa safari ya kwenda na kurudi,” aliongeza Kioko.

Katika safari za Bukoba Precision Air itatumia ndege aina ya ATR42-500 iliyobatizwa jina la Bukoba kama ishara ya shukrani kwa watu wa Bukoba.

Kampuni ya ndege ya Precision imedhamiria kutoa huduma bora kwa wateja wake kwa kutumia vifaa vyake vipya na vya kisasa katika soko la biashara ya ndege. Pia kampuni ina mpango wa kupanua mtandao wake nje ya nchi ikiwemo kuanzisha safari kwenda Johannesburg- Afrika Kusini.

Hivi karibuni watanzania watapata nafasi ya kumiliki sehemu ya Precision Air kwa kunua hisa zake katika soko la hisa la Dar es Salaam.

Mnamo mwaka 2006 Kampuni ya Ndege ya Precision na kampuni ya kutengeneza ndege ya ATR walisaini mkataba wa Dola milioni 129 kwa ajili ya ununuzi wa ndege saba mpya katika mpango wake wa kuboresha ndege zake. Ndege ya mwisho kutoka ATR iliwasili Jijini Dar es Salaam mwezi Septemba mwaka jana.

Mkataba huu wa kibiashara wa ndege hizi saba (2 ATR 42-500 na 5 ATR 72-500) iliwezesha Precision Air kutunukiwa kwa zawadi mbili za kimataifa. Mwezi Aprili 2009, Jarida la AirFinance lilizawadia mkataba huu kuwa Mkataba wa kibiashara bora zaidi kwa Afrika katika mwaka 2008. Mkopo wa ndege za ATR ulikuwa umeshazawadiwa Desemba mwaka juzi na Gazeti la Usafirishaji Jane’s Finance, kama “Mkopo mkubwa wa mwaka Afrika wa ndege 2008.”

Kuletwa kwa ndege hiyo ya mwisho mwezi Septemba imefanya kampuni hii ya ndege kuwa na jumla ya ndege kumi, saba kati ya hizo ni mpya kabisa. Kampuni ya Precision Air pia inatumia ndege moja aina ya Boeing 737.

Kampuni hii ya ndege ina mtandao mkubwa wa safari za anga ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Kigoma, Tabora, Musoma.


 Kioko pia alizungumzia Kampuni yake kujenga hanger lao maalum la kuhifadhia ndege zao na pindi litakapo malizika mapema Mwezi machi litakuwa kama hivi. Mabpo ujenzi wake unaendelea katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.
Kwa sasa jengo hilo linaonekana hivi wakati ujenzi unaendelea.
Posted by MROKI On Tuesday, February 01, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo