MKUTANO MKUU MAALUM WA BARAZA KUU LA SKAUTI TANZANIA KUFANYIKA TAREHE 4 - 5 FEBRUARI 2011.
Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Skauti Tanzania utafanyika Bagamoyo Pwani kuanzia tarahe 4 hadi 5 Februari 2011. Mkutano Mkuu huu pamoja na mambo mengine utajadili na kupitisha Marekebisho ya Katiba ya Chama cha Skauti Tanzania iliyokuwa ikitumika tangu mwaka 1997.
Mkutano huu pia utachagua majina matatu ya wagombea nafasi ya Skauti Mkuu wa Tanzania . Skauti Mkuu huteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Skauti nchini., na hushikilia wadhifa huo kwa muda wa miaka 4.
“Awali nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Kanali [Mstaafu] Iddi Kipingu ambaye muda wake uliisha tangu mwezi Juni 2010. Wagombea wote wa nafasi hiyo watajadiliwa na Kamati ya Utendaji ya Taifa kabla ya kupelekwa katika Baraza Kuu kwa ajili ya kupigiwa kura, ”
Wajumbe wa Baraza Kuu la Skauti ni Makamishna wa Skauti wa Wilaya na Mikoa yote ya Tanzania . Wajumbe hao wametakiwa kufika jijini D’salaam Tarehe 3 Februari 2011 tayari kwa Mkutano huo utakaanza Tarehe 4 Februari na kumalizika Tarehe 5 Februari 2011.
Wajumbe wengine ni Wenyekiti wa Baraza la Skauti la Wilaya na Mikoa [Local Association], Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Taifa, pamoja na Wakufunzi ambao pia hudhuria.
HIDAN .O. RICCO.
KAMISHNA MKUU MSAIDIZI
MAWASILIANO NA HABARI.
SIMU: 0715 019288
0 comments:
Post a Comment