Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa Vodacom Tanzania Upendo Richard akionyesha simu maalum kwa waandishi wa habari ambayo kampuni hiyo imeizindua leo kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuona na kusikia,kushoto Meneja mawasiliano wa kampuni hiyo Nector Foya,kulia Msimamizi wa kitengo cha mauzo wa kampuni hiyo Mgope Kiwanga.
Dar es Salaam January 26, 2011. Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania imezindua simu maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuona na wenye matatizo ya kusikia.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nector Foya, alisema Jijini Dar es Salaam, simu hizo ni tofauti na nyingine kwa kuwa zitawawezesha wateja wao wenye matatizo ya kuona na kusikia kupata huduma ambazo hazipo katika simu za kawaida.
Alizitaja baadhi ya huduma hizo maalum zilizopo katika simu hiyo ni pamoja na maandishi makubwa katika Keypad zake, sauti kubwa katika spika zake na king'ora maalum nyuma ya simu kitakachowawezesha wateja wao kukibonyeza wakati wa dharura.
"Simu hizi za aina yake zitawawezesha wateja wetu wenye matatizo kama hayo kupata huduma ambazo hazipatikani katika simu nyingine za kawaida, natoa wito kwa watanzania wenye matatizo kama hayo kuzichangamkia simu hizi" Alisema.
Alizitaja aina hizo za simu kuwa ni S306 ZTE ambazo zitapatikana katika maduka mbalimbali maarufu kama Vodashop au kwa mawakala wa Vodacom waliopo nchi nzima.
"Tumeamua kuja na simu hizi baada ya kugundua kuwa kuna watanzania wengi wanapata matatizo na simu nyingi kutokana na maandishi madogo, sauti ndogo, na kadhalika. Lengo ni kuwasaidia na kuhakikisha ya kwamba wanaendelea kupata huduma za msingi kwa kutumia simu zao za mkononi bila vikwazo vyovyote vidogovidogo," Alisema.
Alisema kwamba simu hizo zinaweza kutumiwa hata na wasioona kwani ikibonyezwa herufi hutoa sauti inayo kujulisha umebonyeza herufi gani. Hivyo basi ni simu maalum kwa watu maalum katika jamii yetu.
Vodacom Tanzania imekuwa ya kwanza hapa nchini kubuni huduma mbalimbali kwani mbali na simu hiyo,Vodacom mapema mwaka jana ilizindua simu inayotumia mionzi ya jua ambayo imekuwa ikisaidia sana wananchi mbalimbali ambao wanapata matatizo ya miundo mbinu ya umeme.
Vodacom pia imewarahisishia mamillioni ya watanzania kupitia huduma ya Vodafone M-Pesa, huduma inayowawezesha wateja kutuma na kupokea fedha kupitia simu zao za mkononi.
Mbali na kutuma pesa kwa ndugu na marafiki wanao tumia mtandano wa Vodacom. Wateja wana watumia jamaa walio katika mitandao mingine hapa nchini.
Alimalizia kwa kusema, leo tuna furaha kuwawezesha wateja wetu kuchati bure kwenye mitandao ya Face Book, the grid na Vodamail. Vodacom Tanzania itaendelea kuboresha huduma zetu mara kwa mara kwa ajili ya wateja wake na wananchi kwa ujumla.
0 comments:
Post a Comment