Nafasi Ya Matangazo

January 21, 2011

Meneja masoko  wa Precition Air  Emillian Rwejuna akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya punguzo la nauli kwa wasafiri za ndege kwenda  na kurudi Visiwani Zanzibar,kushoto Mkurugenzi wa biashara  wa kampuni hiyo Phil Mwakitawa.



 
Precision Air yazindua nauli maalumu ya Sunrise

Dar es Salaam January 21, 2011. Kampuni ya safari za ndege ya Precision leo imezindua nauli maalumu kwa wasafiri wa ndege wa kampuni hiyo kwenda na kurudi Visiwani Zanzibar kuanzia January 20, 2011.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Biashara - Phil Mwakitawa alisema;

“Kwa muda wa miezi mitano ijayo abiria wetu wa kwenda na kurudi Zanzibar watalipa kiasi cha Shilingi 35,000 elfu za kitanzania kwa safari moja, na Shilingi 60,000 elfu za Kitanzania kwa safari ya kwenda na kurudi.”

Pamoja na hayo, kampuni ya ndege ya Precisionair ilianzisha safari za ndege za mapema alfajiri mnamo mwezi Novemba mwaka jana ili kutoa nafuu hasa kwa wafanya biashara kwa kuondoa usumbufu kwa abiaria wake wanaosafiri katika njia hiyo. Safari ya ndege ya mapema alfajiri kwenda Zanzibar inaondoka Jijini Dar es Salaam saa 1.30 alfajiri wakati safari ile ya kutoka Zanzibar kwenda Jinini Dar es Salaam inaondoka Zanzibar saa 2.30 alfajiri. Kuongezwa kwa safari hiyo ya mapema alfajiri inafanya safari za ndege kwenda Zanzibar kufikia nne na zile za kutoka Zanzibar kwenda Dar es Salaam kufikia saba.

“Kwa kuanzishwa kwa safari hii ya mapema alfajiri, kwa sasa ni rahisi kwa abiria kwenda Zanzibar kwa ndege mapema kabla ya shughuli za kibiashara hazijaanza, kuhudhuria miadi pamoja na wale wanaotaka kuwasili Jijini Dar es Salaam mapema”, alisema Mwakitawa.

Kampuni ya ndege ya Precision imedhamiria kutoa huduma bora kwa wateja wake kwa kutumia vifaa vyake vipya na vya kisasa katika soko la biashara ya ndege.

Mnamo mwaka 2006 Kampuni ya Ndege ya Precision na kampuni ya kutengeneza ndege ya ATR walisaini mkataba wa Dola milioni 129 kwa ajili ya ununuzi wa ndege saba mpya katika mpango wake wa kuboresha ndege zake. Ndege ya mwisho kutoka ATR iliwasili Jijini Dar es Salaam mwezi Septemba mwaka jana.

Mkataba huu wa kibiashara wa ndege hizi saba (2 ATR 42-500 na 5 ATR 72-500) iliwezesha Precision Air kutunukiwa kwa zawadi mbili za kimataifa. Mwezi Aprili 2009, Jarida la AirFinance lilizawadia mkataba huu kuwa Mkataba wa kibiashara bora zaidi kwa Afrika katika mwaka 2008. Mkopo wa ndege za ATR ulikuwa umeshazawadiwa Desemba mwaka juzi na Gazeti la Usafirishaji Jane’s Finance, kama “Mkopo mkubwa wa mwaka Afrika wa ndege 2008.”

Kuletwa kwa ndege hiyo ya mwisho mwezi Septemba imefanya kampuni hii ya ndege kuwa na jumla ya ndege kumi, saba kati ya hizo ni mpya kabisa. Kampuni ya Precision Air pia inatumia ndege moja aina ya Boeing 737.

Kampuni hii ya ndege ina mtandao mkubwa wa safari za anga ikiwa ni pamoja na Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibar, Mwanza, Kigoma, Tabora, Musoma, Shinyanga, Mtwara. Kampuni ya Precisionair pia hufanya safari zake za anga katika miji ya Nairobi na Mombasa nchini Kenya na Entebbe nchini Uganda.
Posted by MROKI On Friday, January 21, 2011 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo