Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa akiba wa wafanyakazi Serikalini(GEPF) Daud Msangi(katikati)akielezea huduma za mfuko huo kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kujiwekea akiba kupitia mpango wake wa hiari wa huduma ya M pesa kwenda namba 700200,kushoto Mkurugenzi wa uendeshaji wa GEPF Anselin Peter na kulia ni Mkuu wa mauzo M pesa Vodacom Tanzania,Franklin Bagalla.
Mkuu wa mauzo M pesa Vodacom Tanzania ,Franklin Bagalla(kulia)akifafanua njia mbadala zitakazotumika kwa wanachama na wasio wanachama wa mfuko wa akiba wa wafanyakazi Serikalini(GEPF)kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kujiwekea akiba kupitia mpango wake wa hiari wa huduma ya M pesa kwenda namba 700200,wapili toka kulia Mkurugenzi wa uendeshaji wa GEPF Anselin Peter,Mkurugenzi mkuu wa GEPF Daud Msangi,Meneja mawasiliano wa Vodacom Nector Foya.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wananachama wa mfuko wa Akiba wa Wafanyakazi Serikalini (GEPF) kuchangia kupitia Vodafone M-Pesa
Dar es Salaam, January 13, 2011: Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imeingia makubaliano na uongozi wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini kupitia mpango wake wa Hiari wa kujiwekea akiba (VSRS) kuweza kuchangia katika Mfuko huo kupitia huduma ya Vodafone M-Pesa.
Mkuu wa kitengo cha biashara na mauzo M Pesa wa Vodacom, Franklin Bagalla alisema jana kuwa mpango huo umefikiwa baada ya Vodacom Tanzania kuingia mkataba wa ushirikiano kati yake na GEPF.
Vodafone M-Pesa ni huduma ya kutuma na kupokea pesa kwa kutumia simu za mkononi ambayo hutolewa na Vodacom Tanzania kwa wateja wake kwenda mtandao mwingine wowote Tanzania.
Bagalla alisema kwamba mteja wa Vodacom aliyejisajili na huduma ya Vodafone M-Pesa sasa anaweza kuchangia fedha kwa kutuma mchango wake kwenda namba 700200.
Alisema mpango huo ni sehemu ya mkakati wa Vodacom Tanzania wa kusaidia sekta ya Hifadhi ya jamii na kurahisisha uchangiaji katika akaunti zao.
Vodacom Tanzania ina mkakati wa kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali hapa nchini ili kukuza na kuboresha njia zilizo bora, zenye uhakika na usalama zaidi katika kuboresha huduma za utumaji fedha, alisema.
Kwa kutumia huduma ya Vodafone M-Pesa, uchangiaji wa hiari katika Mfuko wa GEPF ambao unawagusa Watanzania wote wenye uwezo wa kuzalisha kipato akiwa ameajiriwa au amejiajiri hivi sasa utakua umerahisishwa zaidi, Kiwali alitoa wito kwa Watanzania kutumia ipasavyo mpango huu.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa GEPF Bw Daud Msangi aliishukuru Vodacom Tanzania kwa ushirikiano huo ambao alisema una lenga kukuza kiwango cha ubora wa utoaji huduma na kuwarahisishia wanachama namna ya kuwasilisha michango yao kwa urahisi zaidi.
“Kupitia huduma ya M- PESA, wachangiaji wa mpango wa Hiari wa kujiwekea Akiba (VSRS) wataweza kuchangia moja kwa moja bila makato yeyote kwa mchangiaji au mwanachama”, alisema
Alisema kwa kuanzia michango yote itakwenda katika akaunti zao maalum kama kawaida na kukatiwa risiti. Bwana Msangi, alifafanua zaidi kwa kusema lengo kuu la kuanzisha mpango huu ni kuwawezesha watanzania wote wenye uwezo wa kuzalisha kipato halali katika sekta zote za uchumi; zilizo rasmi na zisizo rasmi kujiwekea akiba dhidi ya maafa yatokanayo na kupungua uwezo wa kuzalisha mali kama vile uzee, ajali, kifo au kupoteza ajira na mtaji wa biashara.
Mpango huu utawezesha Watanzania popote walipo hapa nchini kupata fursa ya kujiwekea akiba zao kupitia M-Pesa.
‘Vodacom na Mfuko wa GEPF unawaomba watumiaji wa mtandao huo, kushiriki katika kampeni hii kwa kuchangia kupitia M-PESA, alisisitiza.
0 comments:
Post a Comment