Nafasi Ya Matangazo

November 25, 2010

 Warembo wa haja wanaoshiriki shindano la Unique Model wakiwa katika pozi baada ya kukamilika mchujo.
 Warembo hao wakipata msosi
Zoezi la kuwasaka wanamitindo wenye sifa za kipekee limekamilika jana katika hoteli ya Giraffe ocean view baada ya wanamitindo kumi kupatikana katika mchujo wa awamu ya pili ambapo mchujo wa awali ulifanyika jumamosi iliyopita.

Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi wa Unique Entertainment Methuselah Magese amesema kazi ya kuwasaka wanamitindo hao ilikuwa ngumu sana kiasi ambacho iliwachukua mpaka kusafiri kwenda mikoa ya jirani kama Tanga, Dodoma na Pwani.

Giraffe Unique Model ni shindano la kumsaka mwanamitindo mwenye sifa za kipekee ambapo jula ya washiriki kumi watapanda jukwaani siku ya tarehe 24 desemba katika hoteli ya Giraffe hotel.

washiriki waliopita katika mchujo huo ni Dorah Mhando, Ritah Samwel, Bilkis Suleiman, Carina Suleiman, Asia Dachi, Calorine Mwakasaka, Diana Mainason, Mariam Rabii, Purity Walele na Jackline Giyabe.
Posted by MROKI On Thursday, November 25, 2010 1 comment

1 comment:

  1. Asante Mkubwa.

    Sasa tunakuomba usitusahau Wakubwa wenzio tu pale watakapokuwa ndani ya "BICH WEA" pliiiz.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo