Nafasi Ya Matangazo

November 18, 2010

 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Waziri Mkuu Mizengo Pinda, wakati wa sherehe hizo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo
 Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Martha Mlatta, wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu zilizofanyika kwenye viwanja vya Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo
 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia), Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu Mteule, Mozengo Pinda, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, wakiwa katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma wakati wakimsubiri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete kuwasili mahala hapo kwa ajili ya kumuapisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, zilizofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete, Makamu wake Dk. Mohamed Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maali Seif Sharif, Jaji Mkuu wa Tanzania, Agustino Ramadhan, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Bunge, Anna Makinda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema na Katibu Mkuu, Philemin Luhanjo,  wakiwa katika picha ya pamoja baada ya sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu mjini Dodoma leo

 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na aliyekuwa mgombea Ubunge wa Jimbo la Kawe kupitia tiketi ya NCCR Mageuzi, James Mbatia, katika viwanja vya  Ikuluv ya Chamwino mjini Dodoma leo Nov 18 wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu
 Mke wa Makamu wa Rais, Asha Bilal na Mke wa Rasi,  Mama Salma Kikwete, wakisalimiana na wananchi waliohudhuria Sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda,katika viwanja vya Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo 

 Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, akiteta jambo na George Mkuchika, wakati wa sherehe hizo.
Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Jaji Mkuu Agustino Ramadhan, wakati wa sherehe za kuapishwa Waziri Mkuu zilizofayika kwenye Viwanja vya Ikulu ya Chamwino mjini D
Posted by MROKI On Thursday, November 18, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo