Taarifa za awali zinasema Primtiva alifikwa na mauti wakati alipokwenda Hospitalini hapo kwaajili ya kujifungua ndipo alipopata na shinikizo la damu ghafla na madaktari wa Lugalo walifanya jitihada za kunusuru uhai wake lakini mauti yalifika wakati juhudi hizo zikiendelea.
Bi. Primtiva amefariki wakati Wanahabari wapo katika msiba mwinge wa Mwandishi wa kike wa Shirika la Utangazaji la taifa TBC, Hilda Mtezi kilichotokea mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Gazeti tando hili linaungana na wafiwa wote wakiwamo wanafamilia na Wafanyakazi wenzake wa Mtanzania katika kipindi hiki kigumi cha kuondokewa na mpendwa wao.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE AMINA.






Mungu Ampe pumziko jema...
ReplyDeletePoleni sana waandishi wa habari kwa kuondokewa na mpendwa wenu.
ReplyDeleteMungu ampe pumziko jema