Nafasi Ya Matangazo

April 21, 2010

Kampuni ya Samsung, kiongozi katika teknologia ya utengenezaji wa simu za mkononi imeendelea kujipa changamoto kwa kutengeneza bidhaa na vifaa vyenye vitu vitakavyowafurahisha na kuongeza ujuzi kwa wateja wake.

Kwa ujumla ili kuwapatia bidhaa zenye ubora wa hali ya juu Samsung imeona ni muhimu na vyema kuwalinda wateja wake kabla na baada ya kununua bidhaa za Samsung.

Simu za mkononi zimekuwa ni vifaa muhimu sana vya mawasiliano kwa kila mmoja wetu. Kutokana na mahitaji makubwa ya simu kumekuwa na wimbi kubwa la uingizwaji wa bidhaa bandia pamoja na wizi wa kifaa hicho,Pia kunahitajika huduma ya matengenezo baada ya mauzo wakati simu itakapopata matatizo ya kiufundi kutokana na matumizi ya kawaida.

Samsung imeelewa madhara ya bidhaa bandia,wizi na huduma ya matengenezo na kuamua kuanzisha njia mbalimbali zitakazowasaidia wateja wake kukabiliana na matatizo hayo.

Simu za Samsung tayari imeanzisha huduma inayoweza kumsaidia mtu kuweza kuipata simu yake pindi itakapokuwa imepotea au imeibiwa na kubadilishwa kadi ya simu.

Huduma hii ya tambua mwizi inathaminiwasanana imesaidia watu wengi walioibiwa simu zao kuzipata na hata kuwakamata wezi wa simu hizo. Pia imekuwa ni kigezo kikubwa kwa wanunuzi kuwa makini kwa kukwepa kununua simu zilizokwisha tumika.

Simu zote halisi za Samsung kutoka kwa wasambazaji waliothibitishwa huuzwa na dhamana ya miezi kumi na mbili.Wakati mwingine mtu huweza kupoteza kadi ya dhamana na kwa hali hiyo inakuwa ni vigumu kuthibitisha kwamba simu hiyo ipo ndani ya dhamana kama mtu hawezi kuwasilisha kadi hiyo.

Leo Samsung inajivunia kutanganza kuanzisha mfumo mpya wa dhamana ya miezi 12 nchini Tanzania utakaotambulika kwa jina la E-warranti.


Hii ni teknolojia mpya inayomwezesha mtu kuandikisha simu yake kwenye mfumo wa miezi kumi na mbili pindi napoinunua.

Kinachofurahisha zaidi huduma hii inamruhurusu mteja kuangalia hali ya bidhaa kabla ya kuinunua.Huduma hii itafanya kazi kutokana na kumbukumbu za nambari za siri za simu za Samsung(IMEI) zilizohifadhiwa kwa mji husika.

Kwa mfumo kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno unaweza kuhakiki uhalisi wa simu na dhamana ya miezi kumi na mbili,kama simu imeripotiwa kuibiwa ama kupotea ama ni bandia au sio ya mahali husika.

Pindi mtu anapoisajili simu yake katika mfumo wa E-Warranty inakuwa ni rahisi kupata huduma zilizo chini ya dhamana ya miezi kumi na mbili.Pia kutokana na uwezo wa kutazama hali ya simu mteja anapata uelewa kamili kuwa wanafanya ununuzi usiotambulika.

Hii ni moja wapo ya mafanikio katika kumtengenezea mazingira mazuri mtumiaji wa simu za mkononi ,ambayo Samsung imeadhimia kumlinda mtanzania kuepuka ununuzi wa bidhaa bandia,zilizokwishatumika na kurejeshwa sokoni na zile zisizo ndani ya dhamana ya miezi 12

Ni haki ya mnunuzi kuwa na uhakika kuwa bidhaa anayoinunua ina ubora na iko chini ya dhamana,na pia ni kazi ya muuzaji kumuhakikishia hilo.Hivyo tunawashawishi wamiliki wa simu za Samsung kusajili nambari za imei za simu zao katika mfumo wa E-warranti.

Zaidi tunawapa moyo wateja kuandikisha simu zao.Samsung inatarajia kuendesha promosheni ambayo wateja watakuwa na nafasi ya kujishindia zawadi nono kama vile LCD,Friji na Home thieta.

JINSI YA KUISAJILI SIMU YAKO KWENYE E-WARRANTI
Jinsi ya kuisajili simu yako kwenye E-Warranti,fuata maelekezo yafuatayo

*Tuma ujumbe mfupi wa maneno ufuatao Reg*NAMBARI YA IMEI ##
Kwenda namba -15685

Ikiwa umefanikiwa utapata ujumbe wa uhakiki usemao
Hakikisha uhalisia wa simu yako ya Samsung kabla ya kununua.

Kuhakiki kuwa simu ya Samsung unayotaka kununa kuwa ni halisi au imefanyiwa marekebisho kabla ya kuinunua

Tuma ujumbe mfupi usemao check*IMEI NUMBER #
kwenda 15685

Jibu litakuwa kati ya yafuatayo.

-Uhakiki wa nambari ya IMEI umekamilika Simu hii ni simu halisi ya Samsung-Hii inamaanisha kuwa simu halisi ina dhamana ya miezi kumi na mbili

-Uhakiki wa nambari ya IMEI umekamilika,Simu ilikwisha andikishwa-Hii inamaanisha kuwa simu imekwisha tumika na sio mpya


-Uhakiki wa nambari ya IMEI umekamilika.Simu imeripotiwa kuibiwa-Hii inamaanisha simu hiyo imeibwa.USIINUNUE

-Nambari ya IMEI haitambuliki au simu sio halisi-Hii inamaanisha kuwa simu haina dhamana ya miezi kumi na mbili.
Posted by MROKI On Wednesday, April 21, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo