Rais Jayaka Kikwete akizungumza wakati mkutano wa kujadili namna ya Kuboresha Huduma ya Afya ya Uzazi nchini New York Marekani.
==============
Tanzania inaunga mkono jitihada za Umoja wa Mataifa(UN) za kuweka mkakati wa kimataifa utakaoharakishanchi maskini kufikia malengo namba 4 na 5 yamillennia ambayo yazitaka nchi hizo kupunguza vifovya watoto wachanga na kuboresha afya ya mamawajawazito.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema leo katika kikaocha Wakuu wa Nchi na washika dau katika jitihada zapamoja za kufanikisha na kuhakikisha nchi maskinizinafikia malengo hayo ifikapo mwaka 2015.
Rais Kikwete amependekeza kuwa mkakati huu ujumuishepamoja na mambo mengine; kuzitaka nchi za Afrika nazinazoendelea kwa ujumla kuweka sera za afyaambazo zitatoa kipaumbele kwenye malengo ya 4 na 5 nakwenye sekta ya Afya kwa ujumla, Kuongezaupatikanaji wa nyenzo muhimu kama fedha, mipango namikakati madhubuti, kupata msaada na kuungwa mkonona kutimizwa kwa ahadi ipasavyo kutoka nchizinazoendelea na kuweka utaratibu utakaohakikishaupatikanaji wa huduma za afya kwa urahisi zaidi kwaakina mama na watoto.
“Hata hivyo ili kufanikisha na kufikia malengo namba4 na 5 kunahitaji pia kufanikisha malengo namba 1 na6, kwani sera hizi zinahitaji kutafsiriwa kwavitendo”. Amesema Rais Kikwete.
NB Lengo la 1 linahitaji nchi kuondoa umaskini nanjaa na lengo la 6 kuondosha HIV/AIDS na maradhimengineyo. Kwa ujumla malengo ya millennia yapo 8.
Rais Kikwete ametoa mfano wa Tanzania ambayo, katikakipindi cha miaka mitatu iliyopita imeweka sera namipango kadhaa inayotoa kipaumbele kwenye afya yaMama na Mtoto, ambapo Mwaka 2007 serikali imeweka sera mpya ya afya badala ya ile ya 1992, (NewNational Health Policy) na kuweka mpango wa miakakumi wa Afya ya msingi (Ten-Year Primary HealthServices Programme 2007-2017) pamoja na Mkakati wakitaifa wa kuhakikisha nchi inapunguza vifo vya akinamama na watoto wachanga wa mwaka ( National Roadmapfor Acceleration of Reduction of Marternal, Newbornan d Child Deaths 2008-2015) na Mkakati wa Sekta yaAfya 2009-2015.
Mpango huu pia utahusisha Mkakati wa kupatikana kwanyenzo na pia kulenga katika kuhakikisha mafunzo kwawafanyakazi wa Sekta ya Afya.
Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na hayo nchi maskinizinahitaji kuungwa mkono kwa kiasi kikubwa na nchitajiri kwa kutimiza ahadi zao za misaada ya hali namali kwani nchi maskini hazina uwezo wa kutengabajeti kubwa itakayowezesha kutimiza mahitaji yakufanikisha malengo hayo ya millennia.
Rais Kikwete amesema, katika mpango wa wake wa Afyawa miaka kumi na katika jitihada zake za kufikiamalengo hayo ya millennia, serikali ya Tanzaniaimeamua kujenga dispensary katika umbali wa kilomita5 katika maeneo ya vijijini ili kupeleka huduma yaafya karibu na wananchi, program ambayo ni ya ubiakati ya serikali na wananchi wake.
“Kwa sababu ya umbali tumeongeza kliniki zitakazokuwazinazungukia wananchi (Mobile Clinics) na kuongezahuduma ya pikipiki (Mobile Motor Bike Ambulances)ambazo zinaweza kutumika kuhudumia mama wajawazitokwa dharura “ Rais amesema na kuongeza kuwa tayariserikali inafanyia kazi uwezekano wa kupata pikipiki400 ambazo zitasambazwa kwenye sehemu kadhaa nchini.
Kikao hicho chao cha siku moja kimefanyika katikaMakao Makuu ya Umoja wa Mataifa, Jijini New York chini ya Uenyekiti wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN) Bw. Ban Ki Moon na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu waNorway Bw. Jens Stoltenberg, Makamu wa Rais waIndonesia Bw. Boediono, Waziri wa Uhusiano waKimataifa Bi. Berverly Oda, Waziri wa Afya na Hudumaza Jamii wa Marekani Bi. Kathleen Sebelius naMkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Afya Duniani (WHO)Bi. Margaret Chan.
Mwisho.
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa habari wa Rais Msaidizi.
New York-Marekani
14 Aprili, 2010.
0 comments:
Post a Comment