
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Karatu, Dr. Wilbroad Slaa kwenye ukumbi wa zamani wa Bunge wa Pius Msekwa mjini Dodoma jana. Bunge lilihamia katika ukumbi huo baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya wa Bunge kupata hitilafu.

Askari akihamisha joho la Spika kutoka kwenye ukumbi mpya wa Bunge kwenda kwenye ukumbi wa zamani wa Msekwa baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya leo.

Askari wakihamisha siwa kutoka kwenye ukumbi mpya wa Bunge kwenda kwenye ukumbi wa zamani wa Msekwa baada ya mfumo wa sauti katika ukumbi mpya leo.

Spika wa Bunge Samwel Sitta akiingia kwenye ukumbi wa zamani wa Bunge wa Msekwa baada ya mfumo wa sauti wa ukumbi mpya wa Bunge kupata hitilafu jana.
0 comments:
Post a Comment