Nafasi Ya Matangazo

April 01, 2010

Katibu Mkuu wa Zamani wa KKKT, Amani Mwenegoha, akiwa na Katibu wa UVCCM Kata ya Ngerengere Wilaya ya Morogoro Vijijini, Semeni Kaniki (kulia) wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Morogoro (hawapo pichani) na kutangaza nia ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la Morogoro Kusini Mashariki.

Mwenegoha aliwahi kugombea tena nafasi hiyo mwaka 2005 ambapo alishika nafasi ya kwanza kwa kupata kura za maoni 285 kati ya kura 547 zilizopigwa na jina lake kukatwa katika halmashauri kuu ya CCM Taifa, na kushindwa kugombea nafasi ya Ubunge.
Posted by MROKI On Thursday, April 01, 2010 1 comment

1 comment:

  1. AnonymousMay 02, 2010

    Anafurukuta arudi tena juu. Ndio tatizo la kuwa kwenye limelight kwa muda mrefu. Ukitoka ni vigumu kuishi maisha ya kawaida. Bado mtu utakuwa unajiona mkubwa tuuu na watu wanaogopa kukuajiri. Mimi naona angefanya mambo mengine tu badala ya kung'ang'ania madaraka. Kutoka kweye dini na kuingia kwenye mashindano ya kisiasa ni dalili kwamba huyu ni mtu anayependa madaraka, kwa udi na uvumba!!

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo