Nafasi Ya Matangazo

March 07, 2010

Mashabiki wa Simba waliofika kushuhudia pambano hilo wakiwashangilia wazungu hao! Raia wa kigeni wakiingia uwanja wa uhuru kushuhudia pambano la ligi kuu ya vodacom kati ya Simba na JKT Ruvu wakitafuta nafasi za kuketi ili kushuhudia pambano hilo, lakini kwa bahati mbaya siti zote zilikuwa zimejaa na walipoombwa wakakae jukwaa la pembeni palipokuwa na nafasi ya kuketi walikataa wakidai kule ni upande wa Yanga na wao ni Simba na kuwaacha kikundi cha kidedea wakiwashangilia kwa matarumbeta.
Picha zote na kwa hisani ya babaTau.
Posted by MROKI On Sunday, March 07, 2010 2 comments

2 comments:

  1. Safi sana hiyo, michezo ni kiungo kizuri sana katika matabaka ya binadamu. Waache waje wafurahi tuu!
    Thx Mroki kwa picha na taarifa.

    ReplyDelete
  2. kaka Mroki sikujua kama na wewe unaweza kudanganya labda kama unafanya utani. Wazungu hao ni wanyeji wangu na hawajui chochote kati ya Simba na Yanga...na mimi ambaye Simba naliwapeleka tu uwanjani sababu nilikuwa napenda kwenda kuona mpira nikaona kuwaacha hotelini peke yao siyo vizuri. Kati ya hao ni mmoja tu anayependa na kujua mpira na wengine Noop...ni watu toka Denmark hao.

    Fred

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo