Nafasi Ya Matangazo

March 06, 2010

Katibu Mkuu wa Chama cha Wapigapicha (PPAT) Mroki Mroki (kulia) akizungumza baada ya kuchaguliwa. Wengine kutoka kwake ni Mwenyekiti Mwanzo Milinga, Makamu Mwenyekiti John Badi na Mwekahazina Leah Samike.

CHAMA cha Wapigapicha za Habari Tanzania (PPAT) kimefanya uchaguzi wake Mkuu leo na kumchagu Mwanzo Milinga kuwa Mwenyekiti na Mroki Mroki kuwa Katibu Mkuu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Katika Uchaguzi huo mkuu uliofanyika jana Dar es Salaam, Mwanzo Milinga alichaguliwa kuwa Mwenyekiti kwa kura 13 na John Badi wa This Day na Kulikoni kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kuopata kura 15 na kuwaangusha Leonard Shumbu aliyepata kura sita.

Nafasi ya Katibu Mkuu wa PPAT, imechukuliwa na Mpigapicha wa HabariLeo na Daily News Mroki Mroki alipita kwa kura 19 bila kupingwa baada ya wagombea Emmanuel Hermana wa Mwananchi kijitoa.

Nafasi ya Mwekahazina wa PPAT ilibaki kwa Leah Samike aliyepita nae bila kupingwa huku nafasi ya Mweka hazina Msaidizi ikichukuliwa na Mwanakombo Jumaa wa Idara ya habari Maelezo.

Aidha Katibu Mkuu Msaidizi alichaguliwa Joseph Mpangala wa Star TV na Wajumbe wane watakao unda Kamati ya utendaji zikienda kwa Khalfan Saidi wa The Guardian, Moshi Kiyungi, Mpoki Bukuku wa The Citizen na Ramadhan Tonge Mwalimu wa Picha Chuo cha Uandishi wa Hari TSJ.

Viongozi waliomaliza muda wao ni Mwenyekiti Juma Dihule, Katibu Selemani Mpochi na Mhazini Leah Samike ambaye alitetea nafasi yake.

Chama cha hicho ambacho Mlezi wake ni Rais Jakaya Kikwete, kiliazimia kufanyika kwa mkutano Mkuu wa Uchaguzi baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kufanya hivyo na kudumaza chama na kurudisha nyuma maendeleo ya wapigapicha za Habari Tanzania.

Akizungumza baada ya kufanyika kwa uchaguzi huo, Mwenyekiti Mwanzo Milinga alisema wakati umefika sasa wa wapigapicha za habari kujipanga upya na kutafuta maendeleo kwa kasi ikiwa ni pamoja na kutumia fursa zilizopo.

“Wapiga picha tumekuwa tukipata fusra nyingi za kimaendeleo lakini kwakuwa umoja wetu ulikuwa sio imara tuklishindwa kuzipata na kuzitumia hivyo wakati umefika sasa wa kuzitumia,” alisema Milinga.

Nae Katibu Mkuuu wa PPAT, Mroki Mroki alisema wanashukuru kuchaguliwa na kupewa madaraka hayo na wanaahidi kushirikiana na wanachama na wadau wote wa picha kuboresha hali za wapigapicha za habari nchini.

“Mpigapicha ni mtu muhimu sana katika chombo cha habari duniani kote…gazeti haliwezi kuitwa gazeti kama halina picha hivyo hivyo televisheni bila picha ni redio hiyo, hivyo sisis ni muhimu sana ila tumekuwa tukidhalilishwa na kudharauliwa bila sababau,”alisema Mroki.

Pia mkutano huo kabla ya kufanya uchaguzi ulipitisha marekebisho kadhaa ya katiba yake ikiwa ni pamoja na kuongeza nafasi za viongozi wasaidini na kupunguza idadi ya wajumbe wake wa kamati ya utendaji.

Miongoni mwa changamoto ambazo viongozi wapya wa PPAT wanakabiliana nao ni pamoja na uimarishaji wa chama, usajili wa wanachama wapya na kujipanga kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Tanzania baadae mwaka huu kama chama.
Posted by MROKI On Saturday, March 06, 2010 2 comments

2 comments:

  1. naomba kuuliza kwani michuzi sio mwanachama/ maana na yeye nimpiga picha wa siku nyingi tena maagazeti ya serikali

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo