Nafasi Ya Matangazo

May 02, 2024












Mkuu wa mkoa wa Singida Halima Dendego amewaagiza Waajiri wote mkoani humo kuhakikisha wanaruhusu Mabaraza ya Wafanyakazi kufanyika sehemu za kazi ili kujua changamoto na matatizo yanayowakabili wafanyakazi kwa nia ya kutafutia ufumbuzi haraka matatizo yanayowakabili nia ikiwa ni kuongeza ari na ufanisi sehemu za kazi. 

Mkuu huyo wa mkoa wa Singida ametoa kauli hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika Kimkoa wilayani Ikungi.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema Mabaraza ya wafanyakazi yanafaida kubwa kwa sababu yanarahisisha kujua changamoto za Wafanyakazi zinazoweza kusababisha kuzorota kwa ufanisi wa kazi hivyo changamoto hivyo zikitafutiwa majawabu mapema zisaidia wafanyakazi kuongeza bidii na ufanisi kazini. 

“Mimi sio Muumini wa Watu wanaovunja Sheria hivyo Waajiri Wakatakaokaidi Maagizo yangu nitashughulika nao”Amesisitiza Halima Dendego.

Aidha, Mkuu wa mkoa wa Singida ameonya kuhusu Waajiri ambao hawaruhusu  wafanyakazi wao kuanzisha au kujiunga na Vyama vyama vya Wafanyakazi na kusititiza kuwa jambo hilo ni kinyume cha taratibu na lazima likomeshwe haraka.

Kuhusu, Madeni ya Wafayakazi Mkoani Singida, Mkuu wa mkoa wa Singida Halima dendego amesema mkoa huo unaendelea na mchakato wa kulipa madeni ya wafanyakazi na kusema kuwa Wafanyakazi wa mkoa huo walikuwa wanaidai Serikali zaidi ya Shilingi bilioni 1.9 na mpaka sasa Serikali imewalipa Wafanyakazi zaidi ya shilingi milioni 700.

Amesema dhamira ya Serikali ya kulipa madeni ipo pale pale kinachotakiwa ni uvumilifu tu.
Halima Dendego amewataka Waajiri wahakikishe wanaacha tabia ya kuzalisha madeni mapya ikiwemo kuhamisha watumishi bila stahiki zao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi  Tanzania ( TUCTA) mkoa wa Singida Agnes Lucas ameishukuru Serikali kwa kuendelea kulipa madeni ya Wafanyakazi, upandishaji wa madaraja na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ikiwemo kuwapatia vitendea kazi vya kisasa hali ambayo imesaidia kuongeza ari na uwajibikaji Sehemu za kazi.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano 
Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Singida.
Posted by MROKI On Thursday, May 02, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo