Nafasi Ya Matangazo

February 11, 2010


Mwanamuzi mkongwe nchini Nguza Viking na mwanae Papii Kocha Nguza (Pichani) wamekutwa tena na hatia katika rufaa yao na hivyo kuendelea na kifungo cha maisha jela.

Nguza alihukumiwa kifungo xcha maisha na watoto wake wengine watatau ambao wawili kati yao wameachia huru leo na Mahakama ya Rufani Tanzania baada ya kutokutwa na hatia dhidi ya makosa ya Ulawiti yaliyokuwa yakiwakabili.

Ilikuwa ni vilio kuanzia kwa mtoto mdogo wa Nguza aliyekuwa akiwalilia baba yake na kaka yake na kwa ndugu pamoja na marafiki waliofurtika mahakamani hapo asubuhi hii. Walioachiwa huru leo hii ni Nguza Mbango na Francis Nguza.

Nguza Mbango alikuwa ni mwanamuziki katika kundi la FM Academia Wajelajela gwaa.

Francis Nguza akilia kwa uchungu baada ya hukumu. Inadaiwa Fracis ndio alikuwa mtoto aliyekuwa karibu sana na baba yake walipokuwa jela.
Posted by MROKI On Thursday, February 11, 2010 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo