Dar es Salaam siku kadha zilizopita.
Licha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kukemea tabia ya uchafu katika mitaa ya Dar es Salaam lakini ndo kwanza uchafu umezidi kushamiri hasa katika eneo la Kariakoo. Pichani ni rundo la taka lililopo katika makutano ya mtaa wa Kongo na Uhuru hivi karibuni.Taka hizi zimetolewa lakini wahusika wajirekebishe na kila mara mji uwe safi.
Linachokera zaidi ni kwamba tatizo la "nidhamu ya taka" liko kila mahali. Si tu majiani Kariakoo. Ndani ya vyoo vyetu lipo, kwenye bichi ukeenda watu wanatupa vyupa ovyo, wanajisaidia ali mradi; ndani ya magari utamwona mtu anamaliza kula au kunywa kitu anakirusha tu nje ya dirisha, kiwe chupa au mabaki ya mfupa wa kuku...Na sio tu Bongo yetu. Kila mahali...hasa bara Afrika, Marekani Kusini na Asia.
ReplyDeleteNi kama mtoto mdogo asiyejua kupenga vizuri kamasi lake analilamba akidhani supu au asali.
Nimelipigia pia suala debe hapa:
http://www.kitoto.wordpress.com