Nafasi Ya Matangazo

March 12, 2009

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua dampo jipya la Pugu Kinyamwezi wilayani Ilala akiwa katika ziara ya Mkoa wa Dar es salaam March 11,2009. Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, anayeshughulikia Mazingira, Batilda Burian.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama ukaangaji samaki kwa kutumia gesi katika soko la samaki la Feri wilayani Ilala akiwa katika ziara ya mkoa wa Dar es salaam March 11, 2009. Jiko la gesi limeezwa kluwa ni suluhisho la tatizo la Moshi linaloathiri soko hilo.
Tahadhari: Mtu huyu kama angelikuwa bna Chuki kama ya yule wa Mwinyi, PM angemwagiwa mafuta usoni, wana usalama next time mumsaidie kugeuza zamaki hawa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua bwawa la maji machafu eneo la Buguruni Kisiwani Wilayani Ilala jijini Dar es salaam March 11,2009 akiwa katika ziara ya mkoa wa Dar es salaam .Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Dr. Batilda Burian.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua Kituo Kikuu cha Mabasi yaenedayo Mikoani cha Ubungo jijini Dar es salaam akiwa katika ziara ya mkoa wa Dar es salaam March 12, 2009. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Fabian Massawe na kushoto kwake ni Meya wa Jiji la Dar es salaam, Alhaj Adm Kimbisa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Fabian Massawe (kulia kwake) kukagua eneo la mfereji wa bonde la Mpunga, Msasani jijini Dar es salaam March 12,2009, akiwa katika ziara ya mkoa wa Dar es salaam.
Posted by MROKI On Thursday, March 12, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo