MDAU WANGU METHEW A SENGA AMETOA MWENDELEZO WA SHAIRI LANGU.
Utumbo maarufu sana,wachaga hawatakana
Umenigusa Mroki,nilifikiri wajoki
Mada kuikoki, mabucha kuyashitaki,
Umenena huropoki, uchafu huutaki,
Ingawa utumbo mtamu,mabuchaye ni machafu
Ingawa utumbo mtamu, mabuchaye ni machafu
Unaweza ishiwa hamu,na moyoni kujaa hofu
Unapotoka zako homu, unusapo buchani harufu
Ingawa utumbo mtamu,mabuchaye ni machafu
Utumbo maarufu sana,wachaga hawatakana
Mtori wanajichana,kwa utumbo ule mpana
Na zile ndizi za kichana,na utumbo zawiana
Ingawa utumbo mtamu,mabuchaye ni machafu
Hapa kuna tatizo,linalo leta mzozo
Watendaji ni kikwazo,miji kuwa uozo
Hawa hawana uwezo, Mroki katoa wazo
Ingawa utumbo mtamu,mabuchaye ni machafu
Hatuwezi shika bakora,kuwatimua maofisini
Kalamu ni kitu bora,kuwafanya wawe makini
Waache kudorora,uvivu waweke chini
Ingawa utumbo mtamu,mabuchaye ni machafu
Mazingira watengeneze, semina waelekeze
Mate siye tuyameze, na wengine wawekeze
Mabucha yatengenezwe,usafi yafidikizwe
Ingawa utumbo mtamu,mabuchaye ni machafu
MTUNZI: Mathew Agripinus Senga
Masomoni Dublin, Ireland.
0 comments:
Post a Comment