Nafasi Ya Matangazo

December 18, 2008

HERRY MAKANGE

Mpigapicha wa Kituo cha Televisheni cha Channel 10/DTV Herry Makange(pichani) amefariki katika ajali ya pikipiki iliyotokea Desemba 17 2008 mchana eneo la Tegeta Dar es Salaam akitokea nyumbani kwake kwenda kazini. Habari zilizoifikia blog hii ya jamii zinasema kuwa Makange alikuwa akienda kazini kuripoti baada ya kutoka safari mkoani Tabora akiwa na taasisi ya Vodacom Foundation. Binafsi ninasema msiba huu nimeupokea kwa masikitiko makubwa sana hasa ukizingatia namna ambavyo nilikuwa nikifahamiana na Marehemu tangu tunasoma Pwani Secondary hadai tunakutana tena katika shughuli zetu hizi za habari. Naungana na Watanzania wote kumpa pole Mjane wa Marehemu, mtoto wa Marehemu, mama mzazi wa Marehemu, wanafamilia wote, Wafanyakazi wenzake pale Channel 10/DTV na Magic FM, Hakika tunampenda Herry lakini Mungu anampenda zaidi hadi sasa amemtwaa na kuwa nae karibu zaidi. Herry Makange akiwa kazini...Picha hii nilimpiga rafiki yangu huyi kipenzi katika maadhimisho ya miaka 47 ya Uhuru Uwanja wa Taifa Dar es Salaam majira ya saa 3:11 asubuhi.
Nakumbuka Herry tulipo kutane pale ikiwa ni siku chahe tu tangu aripoti kazini kutoka katika Fungate na kutaniana utani wertu wa kawaida na baadae kukumbushiana mambo mengi yamaisha yetu na kisha kuniambia.." Ndugu yangu namshukuru Mungu kaniepusha na mengi..ajali zote mbaya na iwapo kama nitapata ajali nyingine sasa nafikiri nitakufa" naweza kusema Makange alitabiri kifo chake.

Kwa wanaokumbuka Herry ajali iliyomuondolea maisha yake ni ajali ya tatu, aliwahi kupata ajali ya kwanza na kuumia vibaya sehemu ya kichwa na kuzirai kwa siku kadhaa, ajali ya pili aliipata akiwa na rafiki yetu mwingine Athuman Hamisi (pichani kulia) na kutoka akiwa salama Athumani tu ndio aliumia vibaya kwa kuvunjika uti wa mgongo na hadi hii leo yupo Afrika Kusini kwa matibabu. Naimani ni mpango wa Mungu wanadamu si kitu zaidi yake yeye Muumba. Tumuombee Herry amani na pumziko la Milele.
*Makange amefikwa na umauti ikiwa ni takribani siku 32 tangu afunge ndoa.
TUTAENDELEA KUWAPASHA HABARI ZAIDI JUU YA MIPANGO YA MAZISHI.



Posted by MROKI On Thursday, December 18, 2008 4 comments

4 comments:

  1. Mkwe, habari hizi nimezipata jana na zimenishtua na kunisikitisha sana. Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi Amin

    ReplyDelete
  2. Yaani nimestuka vibaya sana. Ulale mahali pema kaka

    ReplyDelete
  3. Kifo cha huyu kaka kimenishtua sana.
    Kwa kweli alikua mpole na mcheshi sana, sikuamini maskio yangu niliposikia.
    Mungu alilaze pema peponi roho ya marehemu Hery Makange. Amen.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo