Nafasi Ya Matangazo

June 10, 2024




Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam 
Wizara ya Nishati Imewatoa hofu wadau wa sekta binafsi kuwa serikali inathamini mchango wa matumizi yote ya Nishati safi ya kupikia ikiwemo umeme, gesi, na nishati zingine zote ambazo ni rafiki kwa mazingira na afya.

Hayo yamesemwa kamishna msaidizi wa maendeleo ya Umeme Mha. Styden Rwebangila* wakati akimwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mha. Felchesmi Mramba kwenye mjadala wa wadau wa sekta ya nishati waliokutana kujadili na kutathmini üelekeo wa sekta ya Nishati ilipotoka, ilipo, na inapoelekea baada ya utekelezaji wa  bajeti  ya mwaka 2022/2023 sambamba na changamoto zilizopo na namna ya kukabiliana nazo.

‘’Napenda kuwatoa hofu wadau wa sekta binafsi na watanzania kuwa nishati safi ya kupikia  inajumuusha nishati zote na sio gesi pekee kama wengine wanavyodhani’’ Alisema kamishna Rwebangila.

Alisema *Wizara ya Nishati* inathamini mchango unaotolewa na wadau wa maendeleo hususani *Umoja wa Ulaya* kwa kufadhili miradi mbalimbali kwenye sekta ya nishati hususani nishati safi ya kupikia na itaendelea kushirikiana nao kwenye upangaji wa mipango *mkakati* na uendelezaji wa sera.

Nae Meneja mradi wa Nishati kutoka umoja wa ulaya Massimiliano Pedretti amesema *Umoja wa Ulaya* utaendelea kufadhili miradi ya nishati safi ya kupikia kupitia*mfuko* maalumu wa nishati safi kulingana na mkakati  na utekelezaji kufikia azma ya asilimia 80 ya watanzania kutumia Nishati safi ifikapo 2034 kuunga mkono jitihada za Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Alisema ili Tanzania iweze kufikia azma yake ni lazima ichukue jitihada za makusudi kuhakikisha inaweka mazingira mazuri kwa wauzaji wa mitungi ya gesi, watengenezaji wa wa majiko ya Umeme ili kuchochea wananchi kutumia nishati  safi ya kupikia kwa gharama Nafuu na upatikanaji wa haraka.

Tayari mradi wa mfuko maalumu wa  nishati  safi ya kupikia unafanya kazi na wizara ya Nishati ili kuhakikisha taasisi Kama magereza, shule, hospitali kupitia wakala wa Nishati  REA wanafanya kazi kwa pamoja na kuweka miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwenye maeneo yao.

Kwa upande wake Meneja mradi wa matumizi bora ya Umeme kutoka Shirika la UNDP Aaron Cunningham amesema kuwa *UNDP* iliamua kuunga mkono jitihada za serikali ya Tanzania kwenye sekta ya Nishati safi ya kupikia kwa kuhakikisha pia inaanzisha programu hiyo ili kuwe na matumizi bora ya nishati ya Umeme kwenye Vifaa vitakavyotumiwa na wadau na kuongeza kuwa tayari wameshaainisha viwango vtakavyotumiwa kwenye bidhaa aina tano kama vipoza Umeme,Jokofu, Televisheni, Feni,na majiko ya Umeme ili vitumie Umeme kidogo.

Amesema mradi huu unatekelezwa kwa pamoja na wizara ya Nishati tangu walipoanzisha mwaka 2022  na wamekuwa bega kwa  bega na shirika la viwango Tanzania TBS ili viwango hivyo vitoe unafuu wa matumizi ya Umeme kwenye vifaa hivyo.

Umoja wa ulaya umekuwa Ukichangia kwa Kiasi kikubwa kwenye bajeti na miradi ya maendeleo hususani miradi ya Umeme.

Mkutano huo ulihudhuriwa na taasisi zilizoko chini ya wizara ikiwemo REA,EWURA,TPDC,PURA, TANESCO pamoja na wadau wa maendeleo na sekta binafsi
Posted by MROKI On Monday, June 10, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo