Nafasi Ya Matangazo

May 16, 2024

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akiongoza Kikao cha kwanza cha Kamati ya kuratibu Maandalizi ya Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani leo tarehe 16 Mei, 2024 Geneva nchini Uswisi. (Kushoto ni Katibu Mkuu wa IPU Ndg. Martin Chungong) 
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akiongoza Kikao cha kwanza cha Kamati ya kuratibu Maandalizi ya Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani leo tarehe 16 Mei, 2024 Geneva nchini Uswisi.
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameongoza Kikao cha kwanza cha Kamati ya kuratibu Maandalizi ya Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani leo tarehe 16 Mei, 2024 Geneva nchini Uswisi.

Kikao hicho kilichohusisha Maspika Wawakilishi kutoka Mabunge ya Kanda 6 za Kisiasa na Kijiographia, Wawakilishi kutoka Kamati ya Uongozi, Viongozi wa Makundi ya Wanawake na Vijana pamoja ya Uongozi wa Umoja huo kimejadili kuhusu mapendekezo ya ajenda za Mkutano huo wa Maspika unaotarajiwa kufanyika mwakani na kuona namna changamoto za sasa zinazoikumba Dunia zinavyoweza kuwa sehemu ya ajenda za Mkutano huo.
 
Baadhi ya changamoto zinazotarajiwa kujadiliwa ni pamoja na Mabadiliko ya tabianchi, ukame na njaa hususani Sub Saharan Afrika, machafuko ya amani na vita zinazoendelea  katika baadhi ya mataifa Duniani, usawa wa kijinsia na kujenga Jumuiya jumuishi na za ushilikishwaji. Aidha, mjadala wa demokrasia na matumizi ya akili bandia na matokeo yake nayo ni sehemu ya ajenda zinazotarajiwa.

Posted by MROKI On Thursday, May 16, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo