Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele, akizungumza wakati akifungua mkutano wa siku moja wa Tume na Wadau wa Uchaguzi uliofanyika leo Julai 24, 2024 mkoani Geita.Wadau hao ni pamoja na Viongozi wa vyama vya siasa, Viongozi wa Dini, Wawakilishi wa Asasi za Kiraia, Wahariri wa Vyombo vya habari, Waandishi wa habari, Maafisa Habari wa Mikoa na Halmashauri, Wawakilishi wa Makundi mbalimbali ya Vijana, Watu wenye ulemavu, Wanawake na Wazee wa Kimila.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhan akizungumza na kusisitiza kuwa wapiga kura wanaoboresha taarifa zao wanaweza kuanza mchakato wa awali kwa kutumia simu janja au kiswaswa na kompyuta kupitia mfumo ujulikanao kama Online Voters Registration System (OVRS) au kwa kubobya *152*00#, kisha namba 9 na kufuata maelekezo.

*******************
Na. Waandishi Wetu, Geita na
Kagera
Uboreshaji wa Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura mkoani Geita na Kagera utafanyika kwa siku saba kuanzia
tarehe 05 hadi 11 Agosti, 2024 ambapo vituo vitafunguliwa saa 2:00 asubuhi na
kufungwa saa 12:00 jioni.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele wakati akifungua mkutano wa wadau wa uchaguzi mkoani Geita leo tarehe 24 Julai, 2024.
Meza kuu ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura, Bi.
Giveness Aswile
Viongozi wa kimila ni miongoni mwa wadau muhimu wa Uchaguzi hivyo Tume iliwashirikisha viongozi hao kutoka Kagera.
Wadau kutoka makundi mbalimbali ya wanawake na vijana nao walishiriki.
Makamu Mwenyekiti Wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Mbarouk Salim Mbarouk akiongoza majadiliano wakati wa Mkutano huo.
Viongozi wa kimila ni miongoni mwa wadau muhimu wa Uchaguzi hivyo Tume iliwashirikisha viongozi hao kutoka Kagera.
Wadau kutoka makundi mbalimbali ya wanawake na vijana nao walishiriki.
Wahariri kutoka Vyomb0 vya habari nao walishiriki.
Vyama vya siasa nao walishiriki
Viongozi wa Dini nao walishiriki
0 comments:
Post a Comment