Mbunge wa Jimbo la Chalinze a⁷mbaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete ameendelea na ziada yake jimboni na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Katika ziara hiyo Kikwete ametembelea Kata ya Mikono katika kitongoji Cha Machala na kujionea maendeleo ya ujenzi wa Zahanati inayojengwa pamoja na miradi ya maji.
Miradi mingine aliyotembelea ni miundombinu ya mazingira ya wanafunzi (shule), kwa maendeleo ya wanajamii.
Akizungumza katika vijiji vya Mihuga, Kikaro na Miono Kikwete akisisitiza juu ya Usimamizi Bora wa miradi na ushirikishwaji wa wananchi Ili kuleta tija.
Aidha akiwa katika kijiji Cha Miono alipata nafasi ya kuona maandalizi ya upanuzi wa kituo cha afya na kuzungumza na wataalamu ambapo, aliishukuru Serikali kwa kuleta fedha Sh. Milioni 149 kwaajili ya ujenzi wa Jengo la mama na mtoto.
Pia alipata wasaa mwingine na kwenda kutizama ujenzi wa madarasa 6 na mabweni 4 katika sekondari ya Miono ambapo nimefurahishwa na kuwapongeza kwa Hatua mbalimbali walizofikia.
0 comments:
Post a Comment