Mtaalam wa Astronomia (Astronomy) kutoka
Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Dk.
Noorali Jiwaji wa Kitivo cha Sayansi, Teknologia na Elimu ya Mazingira,
akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) wakati wa kuelezea tukio hilo leo
Juni 22.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa chuo hicho kikuu
Huria, Profesa Elifas Tozo Bisanda.
Mtaalam wa Astronomia (Astronomy) kutoka Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) Dk. Noorali Jiwaji wa Kitivo cha Sayansi, Teknologia na Elimu ya Mazingira, akizungumza na wanahabari (Hawapo pichani) wakati wa kuelezea tukio hilo leo Juni 22.2016, Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa chuo hicho kikuu Huria, Profesa Elifas Tozo Bisanda.
Muonekano endapo
mtumiaji atatumia kichujia jua maalum.
Ramani ya Tanzania
inavyoonesha itakavyokuwa siku tya tukio.
*************
TUKIO kubwa la angani la kipekee la kupatwa kwa
jua usawa wa Tanzania litatokea Septemba 1, 2016, kuanzia saa 4:17 asubuhi hadi
Saa 7:56 adhuhuri.
Washabiki na wanataaluma wa anga kutoka duniani
kote pamoja na wanasansi, wanafunzi pamoja na jamii ya watanzania wataelekea
Rujewa, kusini mwa Tanzania, Karibu na Mkoa wa Mbeya kushuhudia duara la jua
linavyobadilika kuwa pete ya jua. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
Nchini kote Tanzania mamilioni ya watu watashangaa
kuona jua kali la utosi likimegwa kwa zaidi ya asilimia 90 kwa kufunikwa na
mwezi katika kupatwa kwa jua lionekane kama hilali nyembamba au kama mwezi
mwandamo.
Katika tukio hili la kupatwa kwa jua, watu
wanaoishi ndani ya ukanda wenye upana wa kilomita 100 unaokatisha Kusini ya
Tanzania kutoka Congo kuelekea Katavi, mbeya, Ruvuma hadi Masasi na kuingia
Msumbuji, siku hiyo jua kama duara jembamba kama pete kwa vile asilimia 98 ya
jua litakuwa limejificha nyuma ya mwezi.
Kupatwa huko kwa jua kunaweza kuonekana kwa
usalama na watazamaji, lakini inabidi kutumia vichuja maalum vya mwanga wa jua.
Tukio la kupatwa ni la kusisimua na la nadra sana
kutokea katika maisha ya mtu. Hasa kwa kizazi hiki kipya ambacho kimechangamka
kitasisimuliwa sana na tukio la ajabu kama hili na watajifunza Sayansi ili
kuelewa kwa nini kinatokea kile wanachokiona.
Kwa hiyo tukio hili linaweza kutumiwa na shule na
taasisi za elimu kuendeleza Sayansi na kuvuta wanafunzi kujiendeleza kisayansi
na hasa kuelewa mizunguko mbalimbali iliyopo katika mfumo wetu wa sayansi
pamoja na anga za juu kwa ujumla. Kuongeza uelewa wa sayansi ni muhimu katika kuelewa
maumbile ya ulimwengu wetu.
Kupatwa huku kutatokea siku ya alhamisi ambapo
wanafunzi wengi watakuwa mashuleni na ni wakati wa masomo.
Kwavile mchakato wote utaendelea kwa saa nne hivi , kati ya Saa 4 asubuhi hadi Saa 8
mchana wanafunzi wataweza kushirikiana
kuangalia na kusimulia na kujadili tukio ili kulielewa vizuri na
kuandika ripoti madarasani kwao.
Tukio jingine kubwa la kupatwa kwa jua kama hili
halitatokea jingine kwa miaka 15 ijayo, kwa hiyo tunahitaji kutumia fursa hili
kwa ukamilifu.
Ili kluangalia kupatwa huko, kila mmoja atahitaji
kutumia kikinga macho kinachochuja mwanga wa jua kiitwacho kitazamia jua. Nihatari sana kuangalia jua kwa macho ya moja
kwa moja au hata kutumia vichujio vingine vya kiza vilivyotengenezwa kibinafsi.
Kitazamia jua maalum ni kifaa rahisi
kilichotengenezwa kutokana na kichuja nguvu ya jua ambacho kinaondoa mionzi
haribifu kwa asilimia 99.999. Miwani hiyo maalum ya jua inaweza kutengenezwa
Tanzania kwa gharama isiyozidi 500/= kila moja, ikiwemo kuchapa fremu za
kadbodi na kichuja nguvu ya jua (polymer filter) kinachoagizwa kutoka Marekani.
Aidha wataalam wanaonya wananchi kutumia tahadhari
kwa kutoanaglia tukio hilo moja kwa moja kwa macho yao kwani ni hatari na
wanapaswa kutumia miwani maalum ya jua iliyotengenezwa maksusi kwa kazi hiyo.
0 comments:
Post a Comment