Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro akizungumza baada ya hafla kuweka saini makubaliano kati ya pande mbili. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,Juma Idd akifafanua umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha,Juma Idd(kulia) akifafanua umuhimu wa ushirikiano kati ya Jiji na kampuni hiyo,kushoto ni Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro. |
Diwani wa Kata ya Moshono ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji ya Jiji la Arusha,Metson Paul(kushoto) akiwa Mwanasheria na Mkurungezi wa kampuni ya Bondeni Seeds Limited. |
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Goodbless Lema akizungumza katika hafla hiyo. |
Halmashauri ya Jiji la Arusha imesaini makubaliano na kampuni ya Bondeni Seeds Limited kupima eneo linalomilikiwa na kampuni hiyo lenye ukubwa wa Hekari 750 ili liwe sehemu ya Master Plan ya Jiji .
Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro amesema wameshawishika kuingia makubaliano hayo na mwekezaji huyo ili kuwezesha wananchi kuishi kwenye maeneo yaliyopimwa yanayoendana na hadhi ya Jiji na kulipatia mapato yanayotokana naupimaji huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji,Juma Idd amesema wamekubaliana na mwenye eneo hilo kulipanga na kuliendeleza kama sheria ya makazi inavyotaka.
"Hatutaweza kuendelea na makazi ambayo hayajapimwa kama Unga Limited ,Ngarenaro na mengine ,Arusha ni eneo lenye umuhimu wake katika sekta ya utalii,madini na ukizingatia hapa ndio Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na taasisi za kimataifa.
Amesema baada ya kusaini makubaliano utekelezaji unaanza mara moja ili kufikia malengo ya kuweka mji uliopangika.
Mbunge wa Arusha Mjini,Goodbless Lema amewataka wananchi wenye maeneo makubwa kushirikiana na uongozi wa Jiji ili maeneo yao yapimwe kuepusha makazi holela na kuwataka waliojenga maeneo ya mabondeni na kwenye vyanzo vya maji kubomoa nyumba zao.
Imeandaliwa na www.rweyemamuinfo.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment