Mgombea nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia cha cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kinachoungwa mkono na vyama vinne vinavyounda UKAWA kutoka Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, Edward Lowassa amerejesha fomu za kuomba kuteuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kugombea Urais katika uchaguzi utakao fanyika Oktoba 25, 2015. Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva ndie aliyepokea fomu hizo na kutangaza rasmi kumteua Edward Lowassa na mgombea mwenza wake Juma Haji Duni kuwania nafasi hizo kupitia vyama vyao.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi akizungumza.
Mwenyekiti wa Tume akisaini fomu hizo...
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akizungumza mara baada ya kupokea Fomu zilizorudishwa na Mgombea
Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni
baada ya kukamilisha mchakato wa kutafuta wadhamini katika Mikoa 10 ya
Tanzania na kutimiza masharti yote ya Uchaguzi, leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam.
Lowassa akitoka ofisi za NEC huku akisindikizwa na viongozi wa UKAWA.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa rasmi na
Tume ya Uchaguzi kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam. Pembeni yake ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni
0 comments:
Post a Comment