Nafasi Ya Matangazo

June 25, 2015



Makamu wa Rais wa Burundi, Gervais Rufyikiri ameondoka nchini humo kwa kile alichodai kukimbia kusumbuliwa baada ya kupingana na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi kutaka kuongeza kipindi cha tatu cha kuitawala nchi hiyo.

Rufyikiri ameiambia kituo cha Televisheni cha France24, kuongeza muhula wa tatu kwa Rais itakuwa ni kinyume cha matakwa ya katiba.

Aidha Msemaji wa serikali ya Burundi amekanusha madai hayo na kusema kuwa Rufyikiri, amesafiri nje ya nchi kwa shughuli za kikazi.

Bwana Rufikiri amesema amekimbilia usalama wake akidai kuwa maisha yake yamo hatarini.

Msemaji huyo wa serikali amesema iwapo bwana Rufikiri ametoroka Burundi ni kwa maslahi yake mwenyewe wala hakuna yeyote aliyemtishia maisha yake.

Pia taarifa zinasema kuwa mbali na Makamu huyo wa Rais lakini pia Spika wa Bunge la Burundi, Pie Ntavyohanyuma hayupo nchini humo na inasemekana amekwenda Ubelgiji kwa matibabu.

Spika huyo pia anadaiwa kupingana na hitaji hilo la Rais Nkurunzinza la kugombea tena.

Tangu mwezi Aprili mwaka huu Burundi inakabiliwa na maandamano ya mara kwa mara na watu kufa kutokana uamuzi wa Rais Nkurunzinza kutaka kugombea tena katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu.
Posted by MROKI On Thursday, June 25, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo