Nafasi Ya Matangazo

February 20, 2015

"Ni kweli mimi ni Albino, nimejikubali na nimeishi maisha yangu yote bila kujali nilivyo. Sijawahi kutumia hali yangu kupata kitu kwa huruma, nimeyapigania maisha yangu na nimepiga hatua.

Leo hii naongea nanyi nikiwa Baba, Mume, Mwandishi Mwandamizi, Blogger, na mengine mengi, lakini hali yangu sasa inaanza kunikwaza.

Haya mauaji jamani, nimejiteua kuwa Balozi, nitatetea, na kusimama mbele ya wenzangu wote wenye hali kama hii, kama ni wanasiasa ama wafanyabiashara, wanataka kutuua kwa maslahi binafsi, mwaka huu HAPANA.

Wanaoniunga mkono mikono juu" Mwisho wa kunukuu.

Nikiwa kama Blogger na Mwanahabari Mwenza wa rafiki yangu na Kaka yangu Kipenzi,Henry Mdimu aliejitolea kuwa Balozi,nanyoosha mkono juu kwa kuunga mkono kupiga vita vikali mauaji ya ndugu zetu wenye Albinism.kwani wao pia ni Binadamu kama tulivyo mimi na wewe.
 
FATHER KIDEVU BLOG NA UONGOZI WAKE WOTE UKIONGOZWA NA MROKI MROKI 'FATHER KIDEVU' UMENYANYUA MIKONO JUU KUUNGANA NAWE ZEE LA NYETI.
 
JAMANI SASA BASI,NA KILA MMOJA WETU AWE MLINZI KWA NDUGU ZETU HAO.
Posted by MROKI On Friday, February 20, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo