Nafasi Ya Matangazo

December 24, 2014



KESHO ni siku ya Siku kuu, pasi na shaka hakuna mtu ambaye halijui hilo.

Siku kuu ya Krisimasi na mwaka mpya ni siku kuu ambazo hufuatana na kwadesturi ya ushirikiano tulio nao hapa nchini siku hizi hatubagui hatuchagui kila mtu hufurahi pamoja na mwenzake.

Furaha hii ni pale wana jamii walio na mirengo tofauti ya kiimani wanapojumuika pamoja na kufurahia, waumini wa dini ya Kikristo walio wengi kesho wanasherehekea kuzaliwa kwa Masia Yesu Kristo.

Lakini kidoogo tujikumbushe kuzaliwa kwa Yesu Kiristo kulikuaje; Maandiko matakatifu kutoka katika Kitabu cha Biblia Matayo 1:18-21 kunaelezea wazi namna Yesu Kristo alivyo zaliwa.

Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla ya ndoa yao, Maria akiwa bado bikira, alipata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Kwa kuwa Yosefu alikuwa mtu mwema hakutaka kumwaibisha mchumba wake Maria hadharani. Kwa hiyo aliamua kuvunja uchumba wao kwa siri. Lakini alipokuwa bado anawaza juu ya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto akasema, “Yosefu mwana wa Daudi, usisite kumwoa Maria mchumba wako kwa maana mimba aliyo nayo ameipata kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Naye atamzaa mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yesu; kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao.”

Tangu kuzaliwa kwa kristo yapata miaka 2000 sasa na kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.

Hii ni siku ambayo wazazi na watoto wao hukaa pamoja na kufurahi kwa kula na kunywa vinono huku watoto tayari wakiwa wamevalia nadhifu na kufurahi. Siku hizi hata waislamu huwapendezesha watoto wao na wao wenye katika siku hii maana nao hupata mialiko kwa ndugu na jamaa zao kufurahi pamoja.

Leo Anko Kidevu nitazungumzia ulinzi wa familia zetu katika siku hii. Ni dhahiri kuwa tulivyo amka salama asubuhi basi sote tunatamani pakuchwe salama.

Tutokapo asubuhi salama majumbani mwetu pasi na shaka kuwa wale tuliowaacha majumbani wanatamani turudi salama na furaha kuzidi.

Tupo wazazi ambao tutawaruhusu watoto wetu kuzunguka mahali hapa na pale kutimiza furaha zao. Tupo wazazi ambao tutaenda na watoto wetu katika fukwe na katika majumba makubwa ya kibiashara palipo na maduka na michezo ya watoto.

Angalizo langu tu ni kuwa na makini na watoto wetu hata na kila mtu mzima amwangalie mwenzake pia tusije tukapotezana ama kwa kugongwa na magari, kuzama majini au kupotea katika mazingira tatanishi.

Pia ningependa kuvisihi sana vyombo vya dola hasa vya ulinzi na usalama wa raia na mali zao, tuyaangalie maeneo yote ya mikusanyiko kwa jicho la tatu.

Siwafundishi kazi katika hili, ila panapojaliwa wasaa wa kukumbushana ni vyema tukakumbushana maana ulinzi na usalama ni wetu sote.

Jicho la tatu linahitajika sana hasa katika majumba makubwa ya biashara kama, Mlimani City, Quality Center, Shopaz Plaza, May Fair Plaza na kwingineko kote ambako wahuni wachache wanaweza tumia mwanya huo na kututia mchanga katika pilau letu.

Kidevu nilipita katika moja ya majengo hayo leo, lakini nilishangaa ulinzi uliokuwapo siku za nyuma baada ya tukio Septemba 21, 2013, pale katika jingo la Westgate jijini Nairobi, Kenya ambako watu wasio julikana walivamia na kufanya dhahama iliyo gharimu uhai wa watu maduka yetu yalikuwa na ulinzi na uingiapo unakaguliwa lakini sasa naona haupo tena.

Si kweli kuwa wahalaifu wamelala bali wanatusoma tu, hivyo tuwe makini na turejeshe ulinzi katika majengo hayo.

Niimani yangu kuwa wote pia tutabeba jukumu lakuhakikisha usalama wetu unakuwepo kwa watumiaji wa vileo kunywa karibu na nyumbani na kuepuka kutumia vyombo vya moto tukiwa tumelewa.

Watoto wasiende kucheza mbali na nyumbani, tutakao pata wasaa tuingie ibadani na kuwatembelea wagonjwa mahospitalini kuwapa faraja.

Anko Kidevu sina la zaidi bali nawatakia siku kuu njema ya X Mass na Mwaka mpya pia.

AMANI YETU -USALAMA WETU NDIO FURAHA YETU
Posted by MROKI On Wednesday, December 24, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo