Nafasi Ya Matangazo

September 14, 2014

Na Mtuwa Salira,EANA
Wajumbe zaidi ya 100 kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wanahudhuria mkutano wa siku mbili wa Jukwaa la Katibu Mkuu wa EAC kuhusu sekta binafasi na vyama vya kirai mjini Entebe, Uganda.
Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni:''ECA:Nyumbani Kwangu,Biashara Yangu''. Mkutano wa kwanza wa aina hiyo ulifanyika, Dar es Salaam, Tanzania na wa pili ulifanyika Nairobi, Kenya.
Naibu Katibu Mkuu wa EAC,anayeshughulikia Uzalishaji na Sekta ya Jamii, Jessca Eriyo alisema kwamba lengo la Jukwaa hilo ni kutoa nafasi kwa majadiliano ya moja kwa moja kati ya Katibu Mkuu wa EAC na Sekta Bnafsi, Vyama vya Kiraia na makundi mengine juu ya namna ya kuboresha mchakato mzima wa mtangamano wa EAC.
Aliongeza kwamba : ''Jukwaa litatoa nafasi ya kujadili juu ya fursa na changamoto zinaopatiakana kutokana na mchakato wa mtangamano na kubadilishina uzoefu.''
Mada mbalimbali zitawasilishwa katika mkutano huo.
Posted by MROKI On Sunday, September 14, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo