Nafasi Ya Matangazo

September 10, 2014



LEO watoto wetu wapatao 808,111 wanamaliza elimu yao ya msngi ya Darasa la Saba nchini kote.

Hii ni idadi tu ya wale ambao wamejisajili kufanya mitihani hiyo kwa mawa huu na Baraza la Mitihani kuwatambua katika takwimu zao hapa nchini kwa mwaka huu wa 2014 lakini huenda vijana waliostahili kumaliza elimu hiyo ingekuwa kubwa zaidi ukilinganisha na wale waliojindikisha darasa la kwanza 2007.

Nimesema watoto wetu wanamaliza kwaklua tu na mimi katika hao 808,111 bimnti yangu ni mmoja wapo wa wanaomaliza leo na kwa enzi zetu sisi wazazazi wao tungejitapa kuwa ni LY ambayo kimsingi kipindi ile tupo ambao tulikua hatuji maana yake bali ni kufuata mkumbo tu kutokana na viingereza vyetu vya Ugoko kutoka Shule ya Msingi Chini ya Mti.

Hahahaaaa! Mimi nilikuwa nafahamu maana yake ni Last Year! Na hii ni kwasababu tu kaka zangu walikuwa wananifundisha watokapo likizo.

Hoja yangu hapa ni juu ya vijana wetu hawa zaidi ya laki nane ambao kesho wanaingia mtaani na kuazia septemba 12 ni raia na wanarudi mtaani.

Sawa tunaamini kuwa wengi wao baadae watafaulu na kujiunga tena na elimu ya sekondari kupitia shule zetu ambazo tumezijenga kuanzia ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa na hata Taifa kama zipo wataenda. Pia wapo watakao pelekwa na wazazi wao shule za St. Kidevu, St. Kazamoyo na St Kenya na Uganda kwa elimu zaidi.

Hivi katika kipindi hiki kifupi cha kusubiri matokeo tunawasaidiaje watoto hawa kuwajengea misingi bora ya kuishi? Ama tunawatupa tena katika vituo vya masomo ya ziada (Tution) am,bazo zimezagaa kila kona ilimradi tu wazazi tusikae na watoto wetu majumbani.

Ndio wapo wazazi ambao wanasema, Ah! Huyu mtoto asinisumbue akisubiri matokea aende Pre-form One na akae huko huko shule. Tena mzazi huyu ndo yule ambaye mtoto wake alikaa shule ya msingi ya bweni kwa miaka 7.

Naimani hiki ndo kipindi cha kukaa na watoto wetu majumbani na kujua tabia zao vyema ambazo wamejifunza huko mashuleni na ikibidi kuzipiga msasa na kuwaweka sawa.
Wale wenzangu na mimi kutoka shule ya Msingi Kinyenze au Kipera wao ni tofauti maana huko hakuna  cha kupelekwa masomo ya ziada au nini ni safari ya kwa bibi au kwa babu ama kwenda mijini hasa Dar es Salaam kwa kaka, mjomba au ndugu wa karibu kuvuta subira ya kusubiri matokeo na kama hana matumaini ya ufaulu na kuchaguliwa hutafutiwa kazi za ndani au vibarua vya kuuza maji na pipi mtaani.

Lakini leo mimi nakumbuka yaliyokuwa yakifanywa miaka yetu na serikali na hili lilikuwa amri ambayo sijui imeishia wapi yarababi. Hivi nyie mlio hitimu miaka ya 1980’s huko hadi 90 nadhani mnakumbuka jinsi ambavyo ukimaliza elimu ya msingi ulikuwa ukifanyiwa.

Ilikuwa ni jambo la lazima kila mhitimu kuwa na shamba japo la nusu ekari ambalo umepanda pamba na shamba lingine la ukumbwa huo um,epanda mazao ya chakula.

Hili najua kwa mijini ilikuwa haliwezekani lakini vijijini kwetu ilikuwa inawezekana sana na ilikuwa inaleta tija katika jamii maana inawafanya vijana hawa wasizurule hovyo na kujiingia katika makundi yasiyo faa.

Hii leo wahitimu wa elimu ya msingi ni watoto sana. Huenda mwenye umri mkubwa kwa sasa ana miaka 13, bado wadogo sana nadhani sisi kama wazazi ipo njia stahiki ya kuwasaidia watoto wetu hawa katika kipindi hiki kigumu.

Tulio mijini na sisi tusiwaite wadogo zetu na ndugu zetu kutoka kijijini kuja mijini kwa lengo la kuwatafutia shughuli za kufanya kwani bado wadogo sana na nitafurahi sana kama tutafanya hivyo kwa kuwapeleka katika masomo ya ziada kujiandaa na kuanza kidato cha kwanza.

Wajifunze vyema lugha ya mawasiliano huko sekondari ambayo ni kiingereza na mambo mengine muhimu. 

Wazazi waepuka sana watoto wao kuwa wazurulaji mitaani na badala yake watafutiwe shughuli za kufanya ili kuepuka kuzalisha vijana wapya wa vijiwebni na watoa lawama kwa kukosa kazi ilahali wao waliamua kukaa kijiweni. 

Wahitimu wito wangu kwenu ni kuwa wavumilivu na wasikivu kwa wazazi au walezi wenu ili mambo yaende sawa wakati tukijipanga ni wapi tunaenda.
Posted by MROKI On Wednesday, September 10, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo