Nafasi Ya Matangazo

April 16, 2014

 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali leo Aprili 16, 2014 ametembelea viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kujionea maonesho ya Miaka 50 ya Muungano yanayoendelea katika vuiwanja hivyo. Miongoni mwa mabanda aliyotembelea ni banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) na pichani ni Makamu wa Rais akikaribishwa bandano hapo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Asangye Bangu.
 Makamu wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilali akisalimiana na watumishi wa HESLB mara baada ya kufika bandani haopo na kupokea maelezo ya shughuli za HESLB ikiwa ni mafanikio, matarajio na changamoto mbalimbali zinazowakabili na jinsi wanavyo jitahidi kukabiliana nazo.
 Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Asangye Bangu akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais, Dk. Mohamed  Gharib Bilali juu ya shughuli za bodi wakati alipotembelea banda la Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu  (HESLB) lililopo katika viwanja vya Mnazi mmoja yanapofanyika maonesho ya Miaka 50 ya Muuungano Dar es Salaam leo.
 Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilali akitoa neno wakati alipotembelea banda hilo.
Baadhi ya watumishi wa Bodi ya Mikopo wakiwa bandani hapo kusubiri wananchi wawape maelezo ya shughuli zao na nini mtu akifanye apate mkopo.
Posted by MROKI On Wednesday, April 16, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo