Nafasi Ya Matangazo

March 24, 2014



Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya  akiwa na Meneja Matukio Kampuni ya Bia Tanzania  TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud Chawene wakikata utepe kwa pamoja kuzindua kisima hicho cha Maji



Afisa uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha fadhila kwa Watanzania.



Baadhi ya wafanyakazi na wananchi wa mji wa Tunduma wakimsikiliza mgeni rasmi 

Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka akiwashukuru kampuni ya Bia TBL kwa msaada wa kisima hicho



Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya  akiwa na Meneja Matukio Kampuni ya Bia Tanzania  TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud  Chawene wakielekea eneo la makabidhiano ya kisima hicho


Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya  wakipeana mikono Meneja Matukio Kampuni ya Bia Tanzania  TBL Kanda ya nyanda za juu kusini Claud kuashiria kukabidhiwa kwa kisima hicho


Kituo cha Afya Tunduma

Kampuni ya Bia Tanzania imetoa msada wa kisima cha maji kwa ajili kituo cha Afya Tunduma chenye thamani ya shilingi milioni 24 chenye uwezo wa kutoa lita 5000 kwa saa.

Afisa uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa kurudisha fadhila kwa Watanzania.

Malulu amesema kampuni yake imetenga jumla ya shilingi milioni 450 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kwa kipindi cha mwaka wa fedha yenye nia ya kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Naye Afisa mipango Mji wa Tunduma Augustino Ngetwa amesema mradi huo utasaidia kumaliza  tatizo la maji hivyo kuwa faraja kwa wagonjwa wanaotumia kituo hicho ikiwa ni pamoja na raia wa nchi jirani ya Zambia.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya  amesema kuwa watahakikisha wanautunza mradi huo ili uwe na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho .

Aidha Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka ameshukuru Kampuni hiyo kwa kutoa mradi huo na hivyo kuwataka wahudumu kuitunza miundo  mbinu  ya maji. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma Elias Cheyo ameitaka kampuni ya bia kupanua wigo wa kusaidia Nyanja nyingine kama vile elimu ili kufanya mji wa Tunduma kuwa na maendeleo zaidi.
Posted by MROKI On Monday, March 24, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo