Nafasi Ya Matangazo

December 12, 2013

Mjumbe  Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  katika Eneo la Maziwa Makuu, Mary Robinson akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa,  baada ya yeye na Bw. Martin Kobler (kulia) ambaye ni  Muwakilishi wa  Katibu Mkuu  katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa  MONUSCO kuwasilisha taarifa zao mbele ya Baraza Kuu la Usalama, katika mkutano wa ndani wa Baraza hilo  uliofanyika siku ya jumatano. katika mkutano huo wakuu hao wawili walielezea kuridhishwa kwao na hali ya kijeshi na kisiasa inavyoendelea katika DRC hususani eneo la  Mashariki ya nchi hiyo. pamoja na mchakato wa utekelezaji wa Mpango Mpana wa  Umoja wa Mataifa kuhusu siasa, amani, usalama na maendeleo katika  DRC na eneo la Maziwa na  matarajio kuhusu mazungumzo ya Kampala ( Kampala Talks)
**********
Na Mwandishi  Maalam
 Baada ya kundi la waasi la M23 kudhibitiwa ipasavyo na Jeshi la Umoja wa Mataifa linalotuliza amani katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ( MONUSCO) na ambalo ndani yake  kuna Brigedi Maalum ( FIB). Jeshi hilo sasa linaelekeza nguvu zake  katika  kulishughulika  kundi jingine la FDLR.

  Nilipata fursa leo ( jumatano) ya kutoa taarifa  mbele ya    Baraza Kuu la Usalama  kuhusu  maendeleo ya kijeshi na kisiasa katika  DRC. Kwa upande wa kijeshi,  baada ya  mapigano yaliyopelekea kudhibitiwa kwa kundi la M23 sasa MONUSCO imeelekeza  nguvu  zake kwa  makundi mengine ya waasi  na kwa kuanzia tumeanza na kundi la FDLR ( Democratic forces for the liberation of Rwanda)”

Hiyo ni kauli na   Bw. Martin Kobler  Mwakilishi Maaluma wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa MONUSCO.

Alikuwa akiwaeleza waandishi wa habari mara tu baada ya  yeyé  na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu katika Eneo la Maziwa Makuu,  Bi. Mary Robison kumaliza kutoa taarifa zao mbele ya Baraza Kuu la Usalama  lililoketi katika  mkutano wake wa ndani uliofanyika siku ya Jumatano  hapa Makao  Makuu ya Umoja wa Mataifa.

“Tulianza  kulishughulikia kundi la FDLR  Novemba 27, na kati ya   jana na juzi ( disemba tisa na kumi) kumekuwapo  na hatua kubwa zinazofanyika  za kusafisha maeneo  na mitaa muhimu ambayo  inashikiriwa na  FDLR. Tunaendelea na  kazi hii  ambayo ni muhimu sana ya kupambana na makundi yote ya waasi likiwamo  hilo la FDLR  pamoja na  kundi  jingine la ADF (  Allied Democratic  Forces )ambalo lilo katika eneo la Magharibi sana”. Akasema Bw. Kobler

Akasema  kuanzia  hiyo  novemba 27 na  siku za hivi karibu  baada ya eneo la Pinga  ambalo  kwa miaka miwili lilikuwa  mikononi mwa FDRL makundi mengine ya waasi wakiwamo wababe wa kivita   , hivi sasa na baada ya kukombolewa  na njia kufunguliwa kwenda  Goma,  wananchi sasa wanaweza kusafirisha bidhaa zao na kuwatembelea ndugu zao.

Na kuongeza “ Leo nimeleta ujumbe wa matumaini mbele ya Baraza Kuu la Usalama .  Nadhani  hali sasa ni tofauti katika  DRC na hasa baada ya kumaliza  mapigano dhidi ya kundi la M23”.

Akabainisha kwamba  maeneo mengi  ambayo yamekombolewa MONUSCO imeunda   ‘visiwa’  vya  uvulivu  hali aliyosema imeleta matumaini makubwa kwa wananchi, matumaini ambayo yanaonekana bayana katika macho ya wananchi wa maeneo hayo.

 Hata hivyo Bw. Kobler aliyekuwa amefuatana na   Bi. Mary Robison  amesema  bado kuna hati hati lakini  kuna fursa pia,  fursa ya kwamba  baada ya mafanikio haya yote  hali  haiwezi kurejea tena kule tulikotoka na hatuwezi katika miaka michache ijayo  kuanza tena mapigano.
Akafafanua zaidi kwamba nguvu za kijeshi peke yake  hazitaweza kulifanya eneo la Mashariki ya Kongo kuwa na amani na utulivu wa kudumu kwa kile alichosema, utashi na ushiriki kutoka kwa wananchi wa eneo  hilo  ni jambo linalohitajika sana.

Akaeleza zaidi kwamba wananchi wenyewe wanatakiwa  kushiriki katika utatuzi wa  vyanzo ambavyo vimekuwa vikisababisha mapigano na machafuko  ya mara kwa mara akitaja vyanzo hivyo kuwa ni pamoja na  kupigania   utajiri mkubwa wa madini ambao nchi hiyo imejaliwa.

  Kwa kushirikiana na wananchi tunahitaji kufanya kazi pamoja  na kuyashughulikia matatizo yote yanayochangia  migogoro na machafuko, vinginevyo mafanikio ya  kijeshi ambayo yamepatika hivi karibuni yatakuwa hayana maana yoyote na  tutarejea kule  tulikotoka” akasisitiza.

Aidha  Mkuu huyo wa MONUSCO amewambia waandishi hao wa habari kwamba pia amelieleza  Baraza Kuu la Usalama  kuhusu umuhimu wa  mchakato wa waasi kujisalimisha  mchako unaohusisha pia  upokonyaji wa silaha,  usambarishaji wa makundi ya waasi na  uunganishwaji wa waasi hao katika jamii ( DDR).

Amesisitiza kwamba mchanto huo wa DDR ni muhimu sana hasa kutoka  na  dalili za kwamba watu hawaoni tena thamani ya kuendelea na mapigano. “ wanataka kurejea uraiani na kuishi maisha ya  kawaida na huu ni muelekeo mzuri na muhimu hatuna budi kuitumia fursa hii na hasa katika kuwapa matumaini mapya vijana”.

Akafafanua zaidi kwa kusema kwa mfano   asilimia 70 ya   watu katika DRC ni vijana wa umri wa miaka 17 ambao anaamini kwamba wanataka kuwa na maisha bora yenye amani, utulivu na maendeleo.

Akaongeza kuwa baadhi ya wapiganaji wa kundi la FDLR na ambao wengi wao  umri wao ni  chini ya miaka 30 na wamezaliwa baada ya mauaji ya kimbari wanataka sana  kujisalimisha na kwamba  katika miezi ya hivi karibu wamekuwa wakijisalimisha bila ya mapigano yoyote.

Posted by MROKI On Thursday, December 12, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo