Nafasi Ya Matangazo

June 06, 2013


 Jafari Ally enzi za uhai wake akiwa na mkewe Malkia wa Mipasho nchini Tanzania, Khadija Omar Kopa wakifuatilia onesho la Mshauzi Classic ndani ya Mango Garden. 

Habari zilizoufiki mtandao huu hivi punde zinasema kuwa Kijana mtanashati aliyekuwa Mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa, aliyefahamika kwa jina la Jafari Ally, amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa akitibia kile kilichoelezwa alikuwa akisumbuliwa na kifua. 

Jafari na Khadija Kopa, walifunga ndoa mwaka 2008.
 Wakati kifo hicho kinatokea mke wake hakuwepo jijini Dar, kwani alikuwa safarini Rukwa alikokwenda na kundi zima la TOT kwa ajili ya kusherehesha Sherehe za Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika Kitaifa mkoani humo, ambapo leo anatarajia kuwasili jijini. 

Ratiba kamili ya msiba huo bado hadi sasa haijafahamika lakini inadhaniwa huenda msiba huo ukawa  maeneo ya Chaline au Lugoba ambako ni nyumbani kwa wazazi wa Marehemu.
Posted by MROKI On Thursday, June 06, 2013 2 comments

2 comments:

  1. POLENI KWA YALIYO WAKUTA
    2LIMPDA LKN MUNGU KAMPENDA ZAID

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 26, 2013

    Dada Hadidja Poleni saana kwa Muswiba ulio wapata!!!! Mungu amulaze mahala pema mume wako!!!na aukuwa roho ya utulivu na nguvu za kufanya kazi ili ulie watoto.

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo