Wajumbe
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) jana walifanya ziara
katika ofisi za Makao Makuu ya Mfuko huo kwa lengo la kutembelea ofisi
hizo na kuangalia mazingira ya kazi.
Wajumbe
walioteuliwa hivi karibuni wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo,
Balozi Ali Mchumo, Mwanaidi Mtanda, Ezekiah Oluoch, Donan Mmbando,
Mohamed Mohamed, Lydia Choma, Mohamed Hashim, Charles Kajege na Emanuel
Humba ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo.
Wajumbe
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakipata maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Raphael Mwamoto walipozuru
Makao Makuu jana.
Mkurugenzi
wa Uendeshaji, Eugen Mikongoti akitoa maelezo ya namna ya kuhifadhi
kumbukumbu za wanachama katika kituo cha kisasa cha Mfuko huo.
Wajumbe
hao wakipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa NHIF namna ya upatikanaji wa
haraka wa kumbukumbu za wanachama zinazohifadhiwa katika kituo hicho.
Wajumbe wakiendelea kujifunza zaidi katika kituo cha kuhifadhia kumbukumbu.
Mkurugenzi Mkuu Emanuel Humba (wa nne kulia) akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo.
0 comments:
Post a Comment