Nafasi Ya Matangazo

May 07, 2013

KANISA la Katoliki, jimbo kuu la Arusha,jana limetoa tamko la kuitaka serikali iseme ni kina nani wamehusika na tukio la kigaidi la kushambulia kanisa lake la parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasiti huku, likiwataka waumini wa kanisa hilo,kutolipiza kisasi na wawe tayari kushinda ubaya kwa wema.

Katika tukio hilo hadi jana mchana watu wawili na wengine 66 walikuwa wamejeruhiwa na kati ya wanne bado hali zao ni mbaya huku huku wengine 34 wakiendelea na matibabu hospitali ya Mount meru.

Waliofariki  ni Regina Saning’o Losyoki ambaye umri wake haujalikana aliyekuwa muimbaji wa kwaya ya kanisa hilo na  James Gabriel (16) ambaye alifia Uwanja wa Ndege akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Muhimbili .

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha , Josephat Lebulu alitoa tamko hilo, janawakazi akizungumza na waandishi wa habari, akiwa na  Balozi wa Vatcan  nchini Tanzania, Askofu Mkuu Fransisco  Padilla baada ya kuwatembelea majeruhi wa tukio hilo lililotokea juzi.

“Msimamo wa Kanisa katika hili, ni kuwataka waumini wasilipize kisasi  kama ambavyo alisema Yesu kristo kuwa Msilipize kisasi muwe tayari kushinda ubaya jwa wema”alisena Askofu Lebulu,

Alisema maandikio mara zote yanaelekeza kuwa na moyo wa kusamehe lakini pia Serikali inapaswa kuchukuwa hatua kwa wahusika wa maovu.
Hata hivyo alisema lazima serikali iwaambie kina nani wamehusika na watachukuliwa hatua gani.

“tunataka mahakama zitowe maamuzi sahihi  na pia serikali ipambane kuondoa mizizi ya ugaidi”alisema Lebolu.

Alisema kanisa linaamini kuwa waliotekeleza shambulio hilo, walifanyakazi ya shetani na  sio ya waumini wa dini.

Akizungumzia ushauri wa kuongeza ulinzi katika makanisa na maeneo mengine ya Ibada nchini, Askofu Lebulu alisema, kama mioyo ya watu imeoza hata ulinzi ukiwepo matukio ya kigaidi yatakuwepo.

“tunapaswa kujiuliza ni kwanini haya yanafanyika sasa…ingekuwa shambulizi hili limefanywa na mwizi basi tungesema tuongeze ulinzi  lakini hapa ndani ya mioyo ya watu kuna uovu na serikali inapaswa kuondoa mizizi ya ugaidi”alisema Lebolu.

Askofu Lebulu alisema baada ya tukio hilo, wamepokea pole kutoka nchi mbali mbali duniani, ikiwepo Marekani, Italia,India na nyinginezo.

Awali kabla ya kutoa tamko hilo, Balozi wa Vatican Askofu Padilla alitembelea majeruhi katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru na kuwapa pole kisha akawaombea ewapone haraka.

Hata hivyo, licha ya kulaani tukio hilo ambalo alisema ni baya, Balozi huyo wa Vatican hakuwa tayari kuelezea zaidi hatua ambazo wanaweza kuchukuwa kama Kanisa.
 
Askofu Lebulu asimilia kilichotokea kwa Makamu wa Rais
Askofu Lebulu alisema  juzi kabla ya kushambuliwa kanisani, walikuwa ndio wanaanza ibada na hawakujua kilichotokea na alipogeuka yeye na balozi waliona watu wakiwa wamelala chini huku wengine wakilia na kuumia sehemu mbalimbali.

"Hii inasikitisha na watanzania tujiulize kwanini hivi sasa watu wanauwa kama mbwa na kwanini matukio haya yanajitokeza”alisema Askofu Lebulu.

Alisema hajuwi nia ya mhusika aliyelipua bomu alikuwa akimlenga nani kama ni yeye  au balozi na kama si balozi basi huyo mhusika ndio anajua.

“  naskia uchungu sana kwani sijui mtoto yule na mama yule wapo hai au la maana hali zao zilikuwa mbaya sana kwakweli inauma sana''.

Alisema   mhusika aliyefanya tukio hilo ndiye  anayejua alikuwa akimlenga nani lakini hali hii inatisha na akawaomba wakristu wazidi kusali kwani inasikitisha kuona matukio haya yanaendelea.

Alisema wakati tukio hilo, linatokea kulikuwa na kulikuwa na ulinzi wa kutosha wa polisi na awali walifanya na Balozi huyo wa Vatican hadi  Ngorongoro .
“ kwatukio hili linatuhuzunisha sana tena kutokea mbele ya mgeni wetu”alisema Lebulu.
               
Askofu Malasusa atoa tamko
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa, ambaye aliambatana na Makamu wa Rais ,Dk Ghalib Bilal wakitokea mkoani Shinyanga, alisema amesikitishwa sana na tukio hilo.

Alisema tukio hilo sio la kawaida na limewashtua watu wengi wanaopenda amani lakini amewaomba waendelee kuwa watulivu wakati suala hili linapoendelea kufanyiwa uchunguzi.
"Wakristo tuendelee kuhubiri amani, kuombea amani kwa sababu Mungu wetu ni wa amani,"
                      
Makamu wa Rais atoa pole
Naye Makamu wa Rais,Dk Bilal akizungumza baada ya maelezo hayo alitoa pole kwa maaskofu hao na watanzania kwa ujumla kutokana na tukio hilo.

Hata hivyo, aliahidi kuwa Serikali itajitahidi kuhakikisha wote waliohusika na tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya dola.

“serikali inatoa pole kwa tukio hili bay asana lakini tunaahidi tutahakikisha waliohusika kupanga shambulio hili na kutekeleza wanakamatwa”alisema Bilal.

Naibu waziri Nyarandu atoa misaada ya madawa  ya milioni 16 na vyandarua
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu jana alitembelea hospitalini ya Mount Meru na  kuwapa pole majeruhi waliopa madhara mbalimbali akiongozana na viongozi mbalimbali wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Nyalandu alikabidhi msaada wa Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA) kwa waathirika wa tukio hilo wa  mablangeti 50 yenye thamani ya Sh 2.3 milioni  na fedha taslimu kiasi cha Sh 16.2  milioni kwaajili ya kununulia dawa pamoja na vifaa mbalimbali vyakuhudumia wagonjwa hao.

''Nimefika hapa nimehuzunika kwani nimekuta watoto wameumia sana nawapa pole wote waliofikwa na tukio hili na zaidi nawaombea wapone lakini pia nawapongeza madaktari na wauguzi kwa huduma wanazozitoa pia nawaomba na wengine wajitolee kutoa misaada mbalimbali ili kuokoa maisha ya watu hawa'',

Alisema Inasikitisha kuona watoto wakiwa wameumia pamoja na watu mbalimbali lakini zaidi ni mtoto wa miaka mitatu Kelvin Njau ambaye ameumia sehemu za miguu huku mama yake akishindwa kuelezea tukio hilo na kuanza kulia.

Naye  Dk ,Mariam Murtaza ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru aliishukuru wizara kwa msaada huo pamoja na wadau mbalimbali wanaojitokeza kuchangia damu pamoja na vifaa mbalimbali ili kuokoa maisha ya wahanga hao .

Dk Murtaza Pia aliwapongeza madaktari,wauguzi na wataalam mbalimbali kwa ushirikiano wanaoendelea kuuota na kuwaomba waendelee kuwa na ushirikiano kama huo pale yanapotokea majanga mbalimbali.
Posted by MROKI On Tuesday, May 07, 2013 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo