JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
TANGAZO KWA UMMA
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia
Tangazo lake kwenye Gazeti la Habari Leo la tarehe20 Aprili, 2013 siku
ya Jumamosi na la tarehe 23 Aprili, 2013 siku ya Jumanne na kwenye
tovuti ya Wizara, ilitangaza nafasi mbalimbali za kazi za Kada ya Afya
zikiwemo za Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Ustawi wa Jamii Wasaidizi,
Walezi wa Watoto, Maafisa Lishe na Maafisa Lishe Wasaidizi.
Wizara inapenda kuwajulisha waombaji wa nafasi za Kada tajwa hapo juu zitashughulikiwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira.
Hivyo,
waombaji wote waliotuma maombi yao Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
wanajulishwa kuwa maombi yao yatapelekwa Sekretarieti ya Ajira kwa ajili
ya uchambuzi na usaili.
Tangazo
hili halihusu waombaji walioomba Kada mbalimbali za Afya ambazo
zitashughulikiwa moja kwa moja na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Kaimu Katibu Mkuu
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII
22 Mei, 2013
0 comments:
Post a Comment