Nafasi Ya Matangazo

December 20, 2012

WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa leo ametangaza matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba 2012 uliofanyika nchini kote  tarehe 19 na 20 Septemba, 2012.  
Takwimu za matokeo hayo zikionyesha kuwa zaidi ya nusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2013 ni wale waliopata asilimia 40 ya alama kwenda chini katika matokeo hayo.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa wananfunzi 294,833 sawa na asilimia asilimia 52.58  waliopata daraja ‘D’ wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

Hao wanaungana na wenzao 265,873 waliopata madaraja ya A,B na C ambao ni sawa na asilimia 47.41. Kwa mujibu wa taratibu za mitihani ya darasa la saba, jumla ya alama zote ni 250 ambazo zimegawanywa katika madaraja matano ambayo ni A mpaka E.

Mchanganuo wa madaraja hayo ni alama 201 hadi 250 kwa daraja la A, alama 151 – 200 kwa daraja B, alama 101 hadi 150 kwa daraja C, alama 51 – 100 kwa daraja D na alama 0 – 50 kwa daraja E.

Waziri Kawambwa alisema wanafunzi 560,706 walichaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari kati ya 865,534 waliofanya mtihani huo wa siku mbili; Septemba 19 na 20 mwaka huu na kwamba mwaka huu wasichana wamefanya vizuri katika mtihani huo kuliko wavulana.

“Wasichana waliofaulu ni 281,460 sawa na asilimia 50.20 ya  wanafunzi 560,706 wakati wavulana waliofaulu ni 279,246 sawa na asilimia 49.80,” alisema Kawambwa alipokuwa akitangaza matokeo hayo na kuongeza:

“Matokeo yanaonyesha kuwa jumla ya wahitimu 3,087 walipata daraja A, wakati 40,683 walipata daraja la B. Wanafunzi 222,103 walipata alama za daraja C wakati  526,397 walipata daraja D. Watahiniwa waliobaki 73,264 walipata E”.

Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wanafunzi  waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2013, imeongezeka kwa asilimia 8.8 ikilinganishwa na wanafunzi 515,187 waliochaguliwa mwaka jana.


“Mtihani wa mwaka huu, kwa mara ya kwanza watahiniwa walifanya kwa kutumia teknolojia mpya ya Optical Mark Reader (OMR) na ulisahihishwa kwa kutumia kompyuta,” alisema.


Alisema matokeo haya yanaonyesha alama ya juu kabisa ilikuwa 234 kati ya 250 kwa wasichana na wavulana.

Kabla ya matokeo, wasichana waliofanya mtihani walikuwa 456,082 sawa na asilimia 52.68 na wavulana ni 409,745 sawa na asilimia 47.32,” alisema Dk Kawambwa.

“Watahiniwa 29,012 sawa na asiliamia 3.24 hawakufanya mtihani kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo utoro, vifo na ugonjwa,” alisema.

Dk Kawambwa alisema, kati yao, ambao hawakufanya mtihani wasichana walikuwa 12,501 sawa na asilimia 2.67 na wavulana ni 16,511 sawa na asilimia 3.87.

Waziri huyo  alisema,  udanganyifu katika mitihani kwa mwaka huu umepungua kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na idadi ya mwaka jana.

“Waliofutiwa matokeo mwaka huu ni watahiniwa 293 ikilinganishwa na watahiniwa 9,736 waliofutiwa matokeo yao kwa udanganyifu mwaka jana,” alisema Dk Kawambwa.
Katika Mtihani huo Jumla ya wanafunzi 894,881 walisajiliwa kufanya mtihani huo ambapo   wavulana ni  426,285 sawa na asilimia 47.64  na wasichana ni 468,596  sawa na asilimia 52.36. Aidha, kati ya  wanafunzi hao, wapo wanafunzi 874,379  ambao walitarajiwa kufanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na wanafunzi 20,502 walitarajiwa kufanya kwa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo waliyoitumia kujifunzia.  

Wanafunzi wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 92 wakiwemo wavulana 53 na wasichana 39.  Watahiniwa wenye uono hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 495, kati yao wavulana ni 238 na wasichana ni 257.

FATHER KIDEVU BLOG BADO INAENDELEA NA JITIHADA ZA KUPATA LINK YA MAOTOKEO HAYO.
Posted by MROKI On Thursday, December 20, 2012 12 comments

12 comments:

  1. matokeo yanapTIKANA LINK GANI

    ReplyDelete
  2. Fanya mpango wa kutupa hyo link

    ReplyDelete
  3. yako wapi hayo matokeo?

    ReplyDelete
  4. tutashukuru kama m kituwekea link ya kupata hayo majina

    ReplyDelete
  5. mbona hutuwekei hyo link?

    ReplyDelete
  6. Vip mbona tumesubiri sana?

    ReplyDelete
  7. Toka watangaze ni mda sasa sijui utatuwekea lini?

    ReplyDelete
  8. asanteni sana

    ReplyDelete
  9. toeni bas

    ReplyDelete
  10. Ivi Mpaka ulimwengu wa leo Kuna watu wanaamini katika Analogia. Yaani wanashindwa hata hiliiii, Hapana this is too much

    ReplyDelete
  11. Naomba matokeo ya mtihani wa dalasa la Saba MWAKA 2012


    Whatsp namba 0764445959

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo