Nafasi Ya Matangazo

November 01, 2012

 Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Janeth Mbena akitoa hotuba yake wakati wa Uzinduzi wa Kampuni ya Bima ya Afya ya Resolution katika hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Uzinduzi wa Kampuni hiyo umekuja rasmi mara baada ya kupata cheti cha usajili wa kutoa bima ya afya nchini kutoka kwa Mamlaka ya Usimamizi ya Bima (TIRA).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bima ya Resolution,Peter Nduati akizungumza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa Kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam hivi karibuni,ambapo alisema kuwa Kampuni yake imejipanga kufanya mapinduzi katika soko la Tanzania.
Menjea wa Kampuni ya Resolution Tanzania,Oscar Osir akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji kuzungumza na Wadau.
Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima (TIRA), Israel Kamuzora akizungumza kwenye hafla hiyo.
Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Janeth Mbena (kushoto) akiwa pamoja na Mjunbe wa Bodi ya Kampuni ya Resolution,Richard Kasesela wakati wakifuatilia kwa makini taarifa fupi iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya bima ya Resolution,Peter Nduati (hayupo pichani).
 
 
  
 
 
 
 
Baadhi ya Wadau waliohudhulia hafla hiyo ya Uzinduzi wa Kampuni ya Bima ya Afya ya Resolution katika hoteli ya Serena,jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Naibu Waziri wa Fedha,Mh. Janeth Mbena (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Kampuni ya Resolution ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa Kampuni hiyo.
Picha ya Pamoja na Wafanyakazi wote wa Kampuni hiyo ya Resolution.
Posted by MROKI On Thursday, November 01, 2012 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo