Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Bw. Juma Msafiri Karibona, (wa kwanza kushoto aliyekaa), anayefuata ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe. Rashid Hadid Rashid, Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili, Bw. Ali Salim (wa pili kulia) na Afisa Mfawidhi (THBUB, wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya haki za ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa watumishi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, yaliyofanyika Ukumbi wa Wizara ya Fedha, Gombani - Chakechake Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe. Rashid Hadid Rashid (mwenye kofia aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya haki za ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa watumishi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, yaliyofanyika Ukumbi wa Wizara ya Fedha, Gombani - Chakechake Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe. Rashid Hadid Rashid (mwenye kofia aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya haki za ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa watumishi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, yaliyofanyika Ukumbi wa Wizara ya Fedha, Gombani - Chakechake Pemba.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ofisi ya Zanzibar, imewapa elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora, watumishi kutoka taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa mpana watumishi hao ili wawe mabalozi wazuri wa kueneza dhana nzima ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora kwa jamii zao.
Aidha, Bw. Karibona alizisitiza suala la ushirikiano baina ya Tume, taasisi za SMZ na wadau wengine wa haki za binadamu ili kuendelea kulinda na kukuza haki za binadamu na misingi ya Utawala Bora.
Naye, Afisa Mdhamini Ofisi ya Rais Ikulu, Kisiwani Pemba Bi. Shuweikha Abdalla Omar ameishukuru THBUB kwa kuandaa mafunzo hayo na kuisihi Tume hiyo kuendeleza juhudi za kutoa elimu ya haki za binadamu na misingi ya utawala bora katika ngazi zote ili jamii nzima itambue haki na wajibu wao Kisheria.
Kwa upande wake, Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Bw. Ali Salim Matta Mdhamini Alisifu mafunzo hayo na kueleza kwamba yatasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha utendaji wenye uwazi, uwajibikaji, na ushirikiano miongoni mwa watumishi wa umma visiwani humo.
Ufunguzi wa mafunzo hayo ulihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe. Rashid Hadid Rashid, ambaye alionyesha utayari wa mkoa huo katika kuunga mkono juhudi za THBUB katika kusimamia haki za binadamu na kuimarisha misingi ya utawala bora kuanzia ngazi za Shehiya, Wilaya hadi Mikoa.
Wadau wengine waliohudhuria mafunzo hayo ni pamoja na Makatibu Tawala wa Wilaya na Mikoa, Wakurugenzi wa Mabaraza ya Miji, Halmashauri na Manispaa Kisiwani Pemba.










0 comments:
Post a Comment