Nafasi Ya Matangazo

August 04, 2026

Na Neema Chalila Mbuja, Dodoma
NAIBU Mkurugenzi Mtendaji wa SUMA JKT  Brigedia Jenerali  Shija Lupi leo Agosti 03, 2026 ametembelea Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kujionea wadau mbalimbali wanaoshirikiana na wizara kwenye uzalishaji wa bidhaa za misitu na asali na kuipongeza wizara kwa kushirikiana na wadau hao.

Brigedia Jenerali Shija amesema wadau hao wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika kuhakikisha mazao hayo ya bidhaa za nyuki ikiwemo asali, miche ya miti na mazao ya misitu yanakuwa na soko ndani na nje ya nchi.

Brigedia Jenerali Shija alipata wasaa wa kutembelea wanyamapori hai waliopo kwenye Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii kama njia mojawapo ya kuutangaza utalii wa ndani.









Posted by MROKI On Tuesday, August 04, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo