Nafasi Ya Matangazo

May 20, 2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Majaji wa Mahakama ya Rufani. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani ni:-

(i) Mhe. Abdi Shaaban Kagomba – Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,
        Kanda ya Dodoma;
(ii) Mhe. Yohane Bokobora Masara – Jaji wa Mahakama Kuu ya                         Tanzania, Kanda ya Arusha;
(iii) Mhe. Immaculata Kajetan Banzi – Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu         ya Tanzania, Kanda ya Kagera;
(iv) Mhe. Rabia Hussein Mohamed – Jaji wa Mahakama Kuu ya                         Zanzibar;

(v) Mhe. Cyprian Phocas Mkeha – Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya
        Tanzania, Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam;
(vi) Mhe. Yose Joseph Mlyambina – Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya
        Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dar es Salaam;
(vii) Mhe. Imani Daud Aboud – Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania,                 Kanda ya Dodoma;
(viii)Mhe. Mzee Ibrahim Ibrahim – Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar;            na.
(ix) Mhe. Juliana Laurent Masabo – Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu             ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Aidha, uapisho wa Majaji wateule wa Mahakama ya Rufani utafanyika kwa tarehe itakayopangwa baadaye.
Posted by MROKI On Wednesday, May 20, 2026 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo